Na Mwandishi wa A24Tv
Rajabu Mollel ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni wilayani Arumeru Mkoani Arusha amenusurika kuuuwawa kwa mapanga na watu wabaodaiwa kuwa ni ndugu zake wa damu kisa kugombea shamba
Aidha tukio hilo ambalo lilitokea hivi karibuni limewausisha dada,pamoja na watoto Dada mkubwa wa rajabu kutokana na kile kinachodhaniwa kuwa ni mgogoro wa ardhi ambayo iliachwa kama urithi.
Akiongea na waandishi wa habari Bw Rajabu Mollel alisema kuwa mgogoro huo wa ardhi umetokana na urithi ambao alipewa na kaka yake ajulikane kwa jina la Abdi Sulemani ambaye kwa sasa ni marehemu,
Mollel amedai kuwa wakati kaka yake anampa ardhi iyo marehemu kaka yale alifuata taratibu zote za umilikishwaji wa ardhi na mpka sasa nyaraka za umilikishwaji wa shamba hili ambalo lina ukubwa wa hekari moja analo na ni mali yake binafsi .
“Kaka yangu nilikuwa nae kwa kuwa alikuwa ni mgonjwa na alifika hatua ya kunipa shamba hilo kutokana na yeye kutokuwa na mke pamoja na watoto na hivyo aliamua kuniridhisha mimi kaka yeke mkubwa lakini ghafla dada zangu wanangangania shamba hilo ambapo pia hata wazee wa kimila nao kama malegwanani wamekuwa wakichochea mgogoro huu kuwa sehemu mgogoro na Dada zangu waligawa shamba hilo kinyume na utaratibu” aliongeza
Amesema Dada yake Mkubwa aliyejulikana kwa jina la Safia Suleman ndio aliyemtishia kwa mapanga kutaka kumua akishirikiana na watoto wake wa kike wakidai achane na eneo ilo kwakua wamesha pewa na kugaiwa na wazee wa kimila yaani malegwanani wakidai kwamba shamba ilo ni mali ya watoto wa kike kwakua awana maeneo yoyote ya kufikia au kujenga wanapo rudi majumbani.
Mollel ameiyomba serikali kupitia mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Arumeru ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru Enginia Richard Ruyango kumsaidia kwani mpaka sasa anamuda wa siku 5 ajalala nyumbani akiofia kupoteza maisha kwa vitisho anavyo pata kutoka kwa ndugu zake .
A24Tv iliwatafuta Ndugu wa Rajabu kuhusu tuhuma za yeye kulalamikia kuuawa kwake ambapo ndugu yake Safia Sulemani pamoja na Fatuma Sulemani wamekana tuhuma izo za mdogo wao Rajabu kulalamika kwa vyombo vya habari kwamba kutaka kuuawa kwamba sio za kweli kwani wana mgogoro wa uridhi wa eneo ambalo wameliacha mama yao mzazi.
Tofauti na eneo ambalo analalamikia rajabu na kwamba eneo la mama mzazi walipeleka malalamiko mahakamani kwa lengo la kupata mridhi wa miradhi lakini aligoma wito wa mahakama hivyo akuna anaye mtishia maisha kama alivyo sema kwa vyombo vya habari
Ndugu hao wakiwemo Dada zake pamoja na wajomba wamesema kwamba ndugu yao huyo anamatatizo ya akili kwani akuna mtu yoyote aliye mtishia maisha na kutaka kumkata mapanga bali kuna tajiri moja ndiye anaye vuruga familia iyo kwa sasa na kukosa amani
Ndugu hao wamekiri kupewa eneo ilo la ekari moja na viongozi wa kimila ambao ni mailegwanani kugawa eno baada ya vikao vya ukoo bavyo viliketi kwa utaratibu lakini rajabu aliwageuka na kusema kwamba ayupo tayari kuona watoto wa kike wanapata uridhi wa kaka yake mdogo aliyefariki dunia
Ataivyo ndugu hao wamemtaka kaka Rajabu kurudi nyumbani kuacha kukimbia kwani akuna yeyote anayetaka kuatarisha maisha yake kwani uyo ni ndugu yao wa damu na wangependa kumuona anaendelea kua sehemu ya familia yao na kuacha kudanganyika na watu wa nje wasiopenda kuona wako pamoja
Mwisho