Site icon A24TV News

Mkuu wa wilaya ya Arusha aipongeza Ewura

 

Na Geofrey Stephen Arusha .

Mkuu wa wilaya ya  Arusha Arusha ,Said Mtanda ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji  Ewura Mkoa wa Arusha kwa kuandaa mafunzo kwa madiwani wa Jiji la Arusha pamoja na watendaji wa kata wote kwa pamoja kuelimishwa kazi za Ewura .

Mtanda ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa   sekta ya maji uliofanyika jijini Arusha uliolenga kujadili kero mbalimbali zitokanazo na sekta  ya maji ,umeme ambayo ndio matumizi makubwa kwa wananchi ya kila siku ambapo wananchi wengi watahitaji kutambua huduma wanazo pata kama ni sahihi .

Amesema kuwa  madiwani na watendaji wa kata wana nafasi kubwa katika kuwafikishia wananchi ujumbe juu ya huduma wanazo zipata kutoka katika mamlaka ya maji pamoja na Tanesco kwa kutambua huduma wanazo zipata ni sawa na kile wanacho lipia kwani kumekuwepo na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi juu ya bili za maji kuwa kubwa ikilinganishwa na matumizi yao .

Mtanda ameitaka mamlaka  hiyo kuhakikisha inaendelea kutatua kero za wananchi hususani pale wanapo pelekewa malalamiko juu ya huduma ambazo wamekuwa wakizitumia kutoka katika mamlaka usika .

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya udhibiti Huduma za Nishati na Maji Kanda ya Kaskazini Injinia  Lorivii Longidu amesema kuwa  wao kama Mamlaka wameona nafasi kubwa waliyonayo katika jamii ni vyema  kushirikishwa kutambua kazi za mamlaka pamoja na kusaidia kuelimisha wananchi juu ya changamoto wanazo kutana nazo katika huduma za maji na umeme .

Amesema kuwa ,mpaka sasa wamefanikiwa kutatua malalamiko ya wananchi waliofikisha ofisini kwao kwa mwaka wa fedha wa 2021 /2022 zaidi ya changamoto  1500 ambazo zimefanyiwa kazi na wananchi kurejeshewa majibu hususani malalamiko ya matumizi ya ankara za maji kuwa juu .

Longi’du amewataka wananchi wanao kutana na changamoto za kupandishiwa gharama za matumizi ya maji au nishati ya umeme kupanda kwa unit bila kuwepo na taarifa rasmi kufika ofisini kwao na kutoa malalamiko yao  na kuweza kutatuliwa  kwa wakati.

Amesema kuwa, mamlaka hiyo iko kwa ajili ya kutatua changamoto na kuwaelimisha wananchi luhusu huduma ambazo wamekua wakizipata kutoka tahasisi za Mamlaka za maji na Umeme ambazo ndio tahasisi kubwa zinazo wafikia wananchi mara nyingi .

 

Meya wa Jiji la Arusha ,Maxmalian  Iraghe amesema kuwa,pamoja na Madiwani kwa pamoja wamesema mkutano huo umekua chachu ya kutatua changamoto za wananchi wao  na watalua mabalozi wazuri lufikisha ujumbe kwa wananchi ambao wamelua wakiwatumikia latika kata zao ambapo watashirikiana na watendaji wa kata kuwafikia wananchi .

Mwisho