Site icon A24TV News

UJENZI WA SGR LOT 5 CHACHU YA KUFUNGUA MAJIJI YA MWANZA NA DAR

Na Ahmed Mahmoud

Ujenzi unaoendelea wa Reli ya kisasa SGR LOT 5 ISAKA-MWANZA unatarajiwa kufungua biashara Kati ya Mwanza na Dar es Salaam ukikamilika ifikapo mwezi wa 5 mwaka 2024.

Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa Habari waliotembelea Mradi huo wa ISAKA Mwanza Meneja Mradi huo Christopher Kalist Amesema kwamba mradi huo kiuchumi una manufaa na kuwataka wawekezaji kuanza kuwekeza Kwa Sasa.

Aidha alisema Lengo la Serikali kujenga mradi huo ni kufungua biashara za hapa ndani na nje ya nchi ikiwemo mataifa tunayopakana nayo Ili wananchi wapate huduma ya haraka kutoka eneo Moja kwenda jingine.

Kwa mujibu wa Mhandisi Kalist mradi huo kiuchumi utafungua majiji hayo na Mikoa inamopita sanjari jambo ambalo kiuchumi na kimaendeleo ni ukuaji wa miji hiyo kuanzia Lot 1 hadi 5 hivyo nchi kupinga hatua ya kimaendeleo.

Awali Kaimu Meneja wa Mradi huo Moga akiongea kuhusiana na utekelezaji wa Mradi huo ameeleza kwamba umejikita katika maeneo yote kuanzia Ujenzi wa Tuta Reli utunzaji wa Mazingira usalama mahali pa Kazi ikiwemo huduma ya zahanati Kwa wafanyakazi wa Mradi.

Ametaja eneo jingine ni kiwanda cha mataruma malipo ya fidia ya ardhi sanjari na mahusiano ya karibu na wananchi Pamoja na wadau inayowasaidia kuongeza Kasi ya utekelezaji wa Mradi huo.

Anabainisha kwamba Serikali imeendelea Kutoa ushirikiano mkubwa katika kufikia malengo Kwa Kutoa fedha na wao kuendelea kumsimamia mkandarasi kutekeleza mradi huo ikiwa ni ndani ya muda uliopangwa.

Akiongezea Mhandisi Kalist anasema mradi huo wa Lot 5 Kutoka Isaka Hadi Mwanza unajumla ya vituo 10 (Station) ikiwemo Bandari Kavu kituo kikuu Cha kubadilisha vichwa na mabehewa Karakana eneo la Seke nje Kidogo ya Jiji la Mwanza.

Alisema kwamba Mradi huo umepangwa kumalizika ifikapo Mwezi wa Tano mwaka 2024 na ulianza tarehe 15 ya mwezi wa 5 mwaka huu na Kasi yake imefika asilimia 20 ya mradi huo Kwa kuanza majaribio ya utandikaji Reli Kwa mita 150.