WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,wanawake na Makundi maalumu ,dkt Dorothy Gwajima amewataka wahitimu wa taasisi za maendeleo ya jamii (TICD) Tengeru , kuwa mabalozi wazuri wa kupinga vitendo vya ukatili katika maeneo yao, kwa kuwa hali ya ukatili hapa nchini ni mbaya.

Waziri Gwajima alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki ,wakati alipohudhulia mahafali ya 12 katika taasisi hiyo,iliyopo Tengeru wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, ambapo jumla ya wahitimu 1604 walihitimu ,Shahada ya kwanza,Stashahada ya maendeleo ya jamii,Astashahada ya maendeleo ya jamii na  Astashahada ya msingi wa maendeleo ya jamii. 

Aliwaasa wahitimu hao kuitumia taaluma ya maendeleo ya jamii walioipata kwenda kupambana na vitendo vya ukatili nchi nzima,na kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya vitendo vya ukatili vinavyofifisha jitihada za maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.

 

“Baadhi ya jamii zetu zinakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha jitihada za maendeleo ikiwemo mila na desturi kinzani,mmomonyoko wa maadili,ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, kukosekana kwa uzalendo na matumizi ya dawa za kulevya na imani za kishirikina”alisema

Aidha aliitaka taasisi hiyo kuhamasisha wanafunzi kuitikia wito wa wizara wa kuendesha kampeni za kizalendo nchi nzima kupinga ukatili.

Awali mkuu wa Taasisi hiyo ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD) dkt. Bakari George alisema wahitimu 1604 wakiwemo wanwake 1108 walitunukiwa tuzo mbalimbali. 

Alisema kuwa taasisi hiyo imekuwa  ikitekeleza majukumu yake makuu kwa kutoa mafunzo ,kufanya utafiti na kutoa ushauri elekezi kama sheria ya uwanzishaji wa taasisi hiyo inavyotaka.

 

Alisema kuwa taasisi katika kutekeleza majukumu yake inatambua umuhimu wa kuweka uwiano mzuri kati ya nadharia na vitendo ili kuwezesha wanafunzi kuwa na stadi zinazozalisha  ajira.

Dkt George alisema kuwa taasisi hiyo inatilia mkazo utekelezaji wa uanagenzi ,ushirikiano na jamii na ubunifu wa kidigtali .

Naye mwenyekiti wa bodi ya uendeshaji wa TICD dkt.Rosemarie Mwaipopo alisema taaisi hiyo imekuwa ikitekelez miradi mbalimbali baada ya serikali kuipatia fedha .

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kulaza wanafunzib,568 na kumbi pacha za mihadhara.

Alisema septemba mwaka huu taasisi ilipokea fedha za maendeleo kiasi cha sh,bilionin1.6 kwa akili ya ununuzi wa thamanina vifaa vya Tehama.

Aliiomba serikali kuendelea kuipatia fedha taasisi hiyo ili kukamilisha miradi iliyobakia ikiwemo ,jengo la utawala,kituonchabkitaifa cha ubunifu na kumbi ndogo za mihadhara.

Mwisho