Site icon A24TV News

WAZIRI KIJAJI AKUTANA NA MJUMBE WA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA WATETA UWEKEZAJI MKUBWA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.

Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu Fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Masuala ya Biashara Bw. Lord Walney alieambatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo zilizopo Dar es salaam Novemba 30, 2022.

Waziri Kijaji amemhakikishia Mjumbe huyo kuwa Tanzania iko tayali kuendela kushirikiana na Uingereza katika kuendeleza sekta ya biashara na uwekezaji na iko tayali kupokea wawekezaji kutoka nchini humo.