Na Geofrey Stephen Arusha
Waziri wa Malii Asili na Utalii Nchini,Dkt Pindi Chana amezitaka Mamlaka za Hifadhi na Utalii Nchini kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya wa Urithi wa Dunia lengo ni kuvutia Watalii zaidi kuja Nchini kutalii na kuacha kutegemea pekee vyanzo vya zamani.
Alisema hadi sasa Tanzania ina vyanzo saba tu vya Urithi wa Dunia ambapo bado kuna maeneo ambayo bado hayatambuliwa na kuzitaka Mamlaka hizo kukaa na kuja na mpango kazi wa kubuni vyanzo vipya lengo ni kuunga Mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan aliyeagiza kuhakikisha vyanzo vipya vinabuniwa kwa lengo la kuvutia Watalii.
‘’Ninaziagiza Mamlaka za Utalii na Hifadhi kwenda kujifungia na kutoka na mpango kazi wa vyanzo vipya vya Utalii na Hifadhi lengo likiwa ni kutaka kuvutia zaidi watalii’’ alisema Chana
Waziri alisema pamoja na kupanga mpango kazi huo pia shughuli zote hizo zinahitaji Wataalamu wa Urithi wa Dunia hivyo ni wajibu wa Mamlaka hizo kushawishi wanawake kuwa Wataalamu wa fani hiyo tofauti na sasa kwani wengi wao ni wanaume lakini bado hawatoshi kufanya tafiti za Urithi wa Dunia.
Chana alisema kwa Tanzania na Afrika kwa Ujumla watalaamu wengi wa Urithi wa Dunia ni wanaume hivyo ni wajibu wa Mamlaka hizo kutanuwa wigo zaidi kuhakikisha wanawashawishi wanawake kujikita katika fani hiyo ili kuwe na uwiano mzuri.
Alisema wakati umefika kwa Wanafunzi wa Kike wa Vyuo Vikuu vya hapa Nchini kujifunza elimu ya juu ya Urithi wa Dunia ili waweze kuitangaza Nchini ndani na Nje ya Nchi.
Waziri alisema kwa sasa Nchi inaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan,Bunge la Jamhuri wa Tanzania linaongozwa na Spika Dkt Tulia Ackson na Wizara,ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Taasisi kadhaa zinaongozwa na wanawake zaidi ya asilimia 50 hivyo ni wajibu wa Mamlaka kuhakikisha wanatengeneza wanawake wengi kuwa Watalaamu wa Urithi wa Dunia .
Alisema ni heshima kubwa Unesco imeipa Tanzania kwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo wa kwanza kufanyika Afrika kwa kuwa Nchi ililidhia Mkataba wa Kimataifa ni kutokana na kukidhi vigezo vyote vilivyoweka na Unesco katika makubaliano ya utekelezaji wake.
Mkutano huo unaandaliwa na Unesco kwa kushirikiana Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wenye mlengo wa kujadili utekelezaji wa mkataba huo katika masuala ya urithi wa asili na utamaduni kwa kuwaleta pamoja wataalamu mbalimbali kutoka nchi 52 duniani kujadili kwa kina na kuhimniza nchi zinazosuasua kutekeleza mkataba ili ziweze kutekeleza.
Naye Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa{UN} Sekta ya Urithi wa Dunia,Mohamed Juma Mohamed alisema kuwa mbali ya kusherehekea miaka 50 ya Unesco pia wanatoa elimu juu ya Urithi wa Dunia na kuangalia changamoto zilizolikabilia Afrika na kuwa na mipango madhubuti ya kujipanga ili Afrika iweze kuwa na wataalamu wengi katika sekta hiyo.
Afrika bado ina Changamoto ya Wataalamu Kike katika Urithi wa Dunia hivyo ni wajibu wa Mkutano huo kushawishi jinsi hiyo hususani katika Vyuo Vikuu kuhakikisha wanasomea sekta hiyo ili waweze kujikita katika kuitangaza Nchini Kitaifa na Kimataifa.
Naye Kelvin Robert Mkuu wa Kitengo Cha Sayansi Asilia kutoka Unesco Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huu ni kutokana na kuridhia mkataba huu kuanzia kuutekeleza tangu mwaka 1977 pasipokuwa na migogoro ya aina yoyote,
Robert amesema Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ni fursa katika kuleta nchi za kiafrika kufika nchini kujifunza namna njema walivyotekeleza mkataba huo pamoja na kubadilishana changamoto zinazoikabili ikiwemo wataalamu wa kutosha
Tanzania ina jumla ya hifadhi saba zipo katika Urithi wa Dunia ikiwemo Mlima KilImanjaro,Pori la Akiba Selui,Hifadhi ya Serengeti,Mji wa Mawe(Stone town) Zanzibar ,Mapango ya Kilwa Kisiwani,Michoro ya Kondoa{Kondoa Art Work)
Mwisho