Na Mwandishi wa A24Tv Arusha
Afariki dunia baada ya kuchapwa fimbo 280 baada ya kuporomosha matusi ya nguoni mama yake mzazi alikua ni kijana mwenye tabia mbaya ya kutukana baada ya kunywa pombe.
Kijana mwenye umri (32 ) Nelson Mollel mkazi wa sanawari ,Arumeru Mkoani Arusha amefariki dunia baada ya kucharazwa fimbo 70 za kimasai kwa utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la jacline Elias Mollel amesema kijana uyo ametandikwa fimbo 280 badala ya fimbo 70 pamoja na kumwagiwa Tindi kali eneo la kiunoni na kupoteza maisha .
Jacline amesema kwamba Awakatai, wala awabishani na adhabu aliyopewa mdogo wake na Baba yao mdogo Abel Mboya kwa kushirikiana na watu wengine kumi kwa kumchapa kipigo fimbo izo 280 bila kuangalia afya ya kijana huyo kama ni imara .
Ndugu zangu waandishi wa habari atukatai ndugu yetu kuchapwa maana ni mila na desturi zetu sisi wamasai lakini wamezidisha na pia wamemchapa kwa sifa sana wamemvunja mbavu miguu mikono na kumwagia tindi kali chini ya kiuno .
Mama mzazi wa marehemu Elias , aliyejitambulisha kwa majina ya Janeth Kimario amesema kwamba kijana wake alimtukana Matusi ya nguoni siku ya tarehe moja mwaka mpya 2023 na baadae kumwambia baba yake mdogo Abel Mboya (45) ambaye alimwita na kumpeleka porini na kuanza kumchapa fimbo 70 .
“Mama wa marehemu amesema adhabu aliyo pata mwanae ni kubwa sana na ni kweli alistaili kuchapwa kwa kufundishwa adabu pia waandishi niseme tu kwamba awajaniambia mimi adhabu itakua kubwa kiasi cha kumpoteza mwanangu alisema mama wa marehemu “
Pia mama wa marehemu amesema mara baada ya tukio ilo baba mdogo wa marehemu alisha wai kumpiga yeye na kumvunja kidole na kumwambia bado atafanya mauaji kwa wengine iwe fundisho .
Kwa upande wake Enjo Isaya ambaye Marehemu ni Mjomba wake amesema tukio ilo nila kikatili sana hivyo serikali ichukue atua kwa wausika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Arumeru Eng Richard Ruyango amesema wanafahamu utaratibu wa kutolewa kwa adhabu za fimbo 70 lakini kilicho fanyika ni zaidi ya adhabu ya fimbo 70 hivyo ni tukio la mauaji hivyo serikali itawachukulia atua kali walio usika na mauaji ayo
Mwisho .