Site icon A24TV News

BANK YA UBA YAFIKA ARUSHA WAFANYA BIASHARA WAFURAIYA RIBA NAFUU

Na Mwandishi wa A24Tv

Tawi Jipya ndani ya Jiji la Arusha Benki ya United of Afrika (UBA) imezindua Tawi Lake jipya la likiwa ni miongoni mwa matawi 8  ndanibya jijini Arusha,

Ambapo wafanyabiashara katika Jiji la Arusha na viunga vyake wametakiwa kuchangamikia fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu kwa lengo la kukuza biashara

Akiongea Katika uzinduzi wa tawi la benki hiyo iliyopo katika kata ya Levolosi mkabala na Ofisi ya Shirika la nyumba la taifa (NHC),Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango bw.Lawrence Mafuru,kwa niaba ya Waziri wa fedha na Mipango dkt.Mwigulu Nchemba aliitaka benki hiyo kuongeza uwekezaji nchini kutokana na ukubwa wa benki hiyo.

Katibu mkuu Mafuru alisMafuru.wa benki hiyo ni kubwa katika bara la Afrika na Dunia kwa ujumla hivyo ni vema uwekezaji ukaongeza katika bara la Afrika kulingana na ukubwa wa benki hiyo.

“Kwanza niwapongeze kwa hatua ya kuongeza tawi hapa mkoani Arusha lakini ukubwa wa benki yenu ni mkubwa sana mwaka jana niliona ni dola bilioni 27 za marekani,hivyo mna jukumu la kuongeza uwekezaji uendane na benki yenu”Alisema Mafuru.

Aidha alizitaka taasisi zote za fedha kuendelea kuboresha huduma za fedha kwa kuwa ni sekta muhimu ila inakuwa taratibu kwa asilimia chini ya kumi.

Alisema kuwa zipo njia nyingi za kukuza sekta hiyo ikiwemo kuongeza huduma hizo karibu na wanachi na kufungua matawi katika maeneo ya vijijini ili wanachi wahifadhi fedha zao kwa usalama.

Akisoma kwa risala kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo ni Bw.Martin Mmari alisema benki hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbali mbali ikiwemo sekta ya Elimu na Afya kupitia UBA Faundation.

Pia alisema kuwa jumla ya vijana wa kitanzania 200 wamenufaika na mikopo ya ukuzaji wa mikopo.

Nae Mkurugenzi wa UBA Tanzania Gbenga Makinde maarufu kama GMak alisema kuwa benki hiyo imejiwekea malengo ya kuhudumia wafanyabiashara katika bara la Afrika na ina matawi nane sasa.

Matawi hayo ni Dar es salaam manne,Dodoma,Rufiji,Mwanza na Arusha,huku mpango ukiwa ni kusogeza huduma katika mikoa mingine ambayo ni Mbeya,Zanzibar,na Mtwara.

 

Mwisho