Site icon A24TV News

FREEDOM HOUSE KUFANYAKAZI NA MAIPAC

 

Mwandishi wetu, MAIPAC

Arusha.Shirika la Kimataifa la Freedom la House , limeahidi kufanya kazi la taasisi ya Wanahabari ya kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) Ili kutekeleza mpango mkakati wake wa miaka miaka mitano 2020-2025.

Mpango huo wa Maipac (strategic plan) unalenga kusaidia jamii hizo kuchochea maendeleo na kuwezesha wanahabari kuifikia kufanya habari za uchunguzi Ili kutatua changamoto kadhaa ukatili wa kijinsia masuala ya Mazingira na Ushiriki katika masuala ya Kidemokrasia na Utawala bora

Maipac kwa Sasa inatekeleza mradi wa uhifadhi mazingira,vyanzo vya maji na misitu kwa maarifa ya asili ambao unaofadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) kupitia program ya miradi midogo na mfuko wa Mazingira duniani (GEF).

Mradi huo ambao unatekelezwa kwa wilaya tatu za Monduli, Longido na Ngorongoro unaratibiwa na jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) na unashirikisha halmashauri za wilaya hizo na wadau wengine.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Freedom House nchini Tanzania Wakili Daniel Naftali Lema akiwa MAIPAC ameeleza kufurahishwa na Utendaji kazi wa Taasisi hiyo ya kipekee

Akizungumza katika Ofisi za MAIPAC baada ya kukutana na watendaji wa Taasisi hiyo na kupokea taarifa ya utekelezaji miradi m mbalimbali,Lema amesema ameridhishwa na Utendaji wa MAIPAC.

Amesema amefurahishwa baada ya kugundua taasisi hii yenye wanachama kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejikita zaidi katika kusaidia kupaza sauti za jamii hizo za pembezoni na makundi maalum Ili kukabiliana na changamto za ardhi, haki za wanawake na watoto na walemavu .

“Ninawapongeza sana MAIPAC kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuandika habari za uchunguzi zinazosaidia jamii za pembezoni kujua haki zao na changamoto zinazowakabili ili iweze kupatiwa msaada na serikali na taasisi za kitaifa na kimataifa” amesema Na kuongeza

“Nimependa mpango mkakati wenu mnaoutekeleza sasa wa miaka mitatu na tutangalia objective ipi tutakayoona inafaa kupewa sapoti na freedom house ili muweze kuitimiza vema kazi zenu” amesema

Awali akimkaribisha ofisini hapo na kumtambulisha kwa baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo ofisin hapo, Afisa utawala wa taasisi hiyo Andrea Ngobole amemwelezea mtendaju mkuu huyo kuwa taasisi ya MAIPAC ina wanachama 60 nchi nzima, ambao Huandika na kuchambua habari za jamii za pembezoni ili ziweze kusikika na kupatiwa suluhisho la kudumu na wenye mamlaka.

Amemshukuru kwa kutembelea ofisi hiyo na kuwa na dhamira ya dhati ya kujenga mahusiano mazuri kati ya maipac na freedom house katika kutekeleza na kuboresha baadhi ya maeneo yenye uhitaji wa haraka kama uandishi bora wa mpango mkakati na usimamizi wa miradi.

Naye afisa miradi wa MAIPAC Deborah Makando amemuelezea kuwa taasisi imekuwa na maono mapana ya kutatua changamoto nyingi zinazokabali wanawake wa jamii za kifugaji kuwezesha kuwa na kipato endelevu, pia kuondokana na tatizo la ndoa za utotoni zinazowanyima haki ya kupata elimu na kuleta umaskini kwa jamii hizo.


Mwisho