Site icon A24TV News

JAMII YAASWA KUTUNZA WATOTO SIO KUPELEKA VITUO VYA KULELEA WATOTO

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha .

Jamii imeaswa kuacha Tabia ya kuwapeleka watoto ambao wamefiwa na wazazi wao kwenye vituo vya mayatima na badala yake wawatunze ikiwa ni pamoja na kuwapa maitaji muhimu ya Kila siku.

Mtoto Faith Ole Ngereza akikabidhi misaada kwa niaba ya watoto wengine

Endapo kama jamii itaweza kuwasaidia watoto hao kwa njia hiyo basi kutakuwa hakuna ongezeko la watoto yatima lakini pia ongezeko la watoto wa mitaani

Hayo yameelezwa na Wakili Mary Mwita ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha kisheria kijulikanacho kama smart community on legal protection wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wa kituo cha watoto yatima Ungalmt kituo Kinachomilikiwa na kanisa la International Evangelism church kilichopo Ungalmtd Jijini Arusha.

Mtoto Faith Ole Ngereza akikabidhi misaada kwa niaba ya watoto wengine

Wakili Mary alisema kuwa jamii kwa sasa inatakiwa ihakikishe kuwa maitaji ya watoto hasa Yale ambayo ni muhimu wanapata hata kama wazazi wao hawapo tena duniani

Alifafanua kuwa wazazi wanapotwaliwa na Mungu waliobaki Wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanawatunza na kuwajali watoto hata kama sio wao

“Tukifanya hivyo ni wazi kuwa idadi ya watoto ambao wanaletwa kwenye vituo itapungua kwa kiwango embu sasa Kila mtu aone kuwa mtoto wa mwnzako ni wako na Una jukumu kubwa Sana la kuweza kumlinda mpaka afike umri wa kujitegemea”aliongeza

Wakati huo huo alitoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa wanajijengea Tabia ya kuhudhuria kwa watoto wenye maitaji maalumu pamoja na watoto wao ili kuweza kupandikiza mbegu ya Amani na upendo kwa hapo baadae

“Leo nimefuatana na timu kubwa Sana ya watoto ambapo napenda kupandikiza mbegu ya upendo na wajue na kutambua kuwa hili la kuangalia mayatima na wenye maitaji maalumu ni sehemu ya maisha Yao”aliongeza

Akiongea kwa niaba ya watoto ambao walifija kituoni hapo kwa ajili ya kutoa misaada,Faith ole Ngereza alisema kuwa hata watoto wengine wanapaswa kutambua kuwa mayatima ni sehemu ya jamii.

Picha za misaada mbali mbali

Faith alibainisha kuwa mayatima wanaitaji misaada mkubwa na hawatakiwi kuacha wakiwa na shida kwa kuwa hata mandiko matakatifu yanasisitiza jamii kuweza kuwajali mayatima.

Hataivyo misaada iliyotolewa ni pamoja na vifaa vya shule,pamoja na zawadi mbalimbali ambapo baada ya kukabidhiwa kwa misaada hiyo watoto wa kituo hicho kwa kushirikiana na wageni waliweza kushiriki katika michezo mbalimbali.

Mwisho