Site icon A24TV News

KANISA LA KKAM PAROKIA YA NGULELO ARUSHA LAPIGA VITA NDOA YA JINSIA MOJA

 

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha

Kanisa la Kilutheri Afrika ya Mashariki(KKAM) limetoa msimamo wake katika mjadala unaendelea duniani wa ndoa za jinsia moja na utoaji wa mimba kwa kupinga vikali ndoa hizo huku likiweka bayana mipango ya jimbo la Arusha katika kuielemisha jamii kusimama katika maadili.

Msimamo huo umebainishwa na makamu askofu mkuu wa kanisa hilo hapa Tanzania ambaye pia ni askofu wa jimbo la Arusha Dkt.Philemon Mollel wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa halmashauri kuu ya kanisa hilo nchini.

Askofu Mollel amwsema kwamba awawezi kufumbia macho matukio kama ayo kwani jamii kwa sasa imekua na changamoto kubwa sana katika maswala ya ndoa ya jinsia moja jambo ambalo alikubaliki hata kidogo katika jamii ya Tanzania .na Africa kwa ujumla 

Dkt.Philemon Mollel ametaja misingi ya kanisa hilo katika kuhamasisha jamii kuondokana na vitendo mbalimbali vya ukatili kwa binadamu na pia jamii kuacha kuiga vitendo ambayo siyo maadili ya Kitanzania vya ndoa za jinsia moja na ushoga

 

 

Nao wajumbe halmashauri kuu ya kanisa hilo kutoka kwenye parokia za maeneo ya jamii ya wafugaji wanaonya kuhusu baadhi ya tabia zinazochangia kuharibu maadili hususani kwa watoto wadogo

 

Kwa upande wake Msaidizi wa askofu mkuu wa kanisa hilo jimbo la Arusha Dkt.Philemon Olais Monaban anawataka wazazi kuanza kuwachunguza mara kwa mara vijana wao ili kubaini pale wanapobadili tabia na kuwarudisha katika maadili.

 

Mwisho.

Picha kwa hisani ya channel ten