Site icon A24TV News

WAZIRI KIJAJI AZITAKA HALMASHAURI NJOMBE KUKUSANYA MAPATO YA MBAO KWA ASILIMIA 3

 

Na Mwandishi wa A24Tv  Njombe

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe kuhakikisha inakusanya mapato ya Mbao kwa asilimia 3 kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Serikali na siyo shilingi 100 kwa kila ubao kama ilivyo sasa kwa baadhi ya Halmashauri.

Hii ni baada ya wafanyabiashara mbalimbali kuomba Mapato ya ushuru wa Mbao walipe kwa asilimia 3 wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la wafanyabiashara Mkoa wa Njombe wakiwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara unaofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe.