Site icon A24TV News

WAZIRI WA HABARI NAPE NNAUYE AZINDUA MNARA WA SIMU WANGING’OMBE NJOMBE KUBORESHA MAWASILIANO

Na Emmanuel wa A24Tv.

Waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye amesema kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia hakuna budi serikali ikaendelea kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano kwa kujenga minara ya simu inayoweza kusaidia kupunguza adha kwa wananchi.

Nape ametoa kauli hiyo Wakati akizindua mnara wa simu wa Vodacom katika Kijiji cha Kinenulo kata ya Imalinyi Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe uliojengwa kwa ushirikiano na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF na hivyo Ni lazima kuwekaza kwenye mawasiliano ili kuendana na teknolojia hiyo.

Justina Mashiba ni mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF Ambaye anasema serikali imetoa shilingi bilioni 4.8 kwa ajili ya kujenga Minara 32 katika mkoa wa Njombe ambayo inajengwa kwa ubia wa makampuni ya simu.

Magreth Laurance ni mkuu wa kanda ya nyanda za juu kusini toka kampuni ya Vodacom ambaye anasema mnara huo ulikamilika na kuanza kufanya kazi