Site icon A24TV News

ASKOFU MASANGWA AKUTANA NA UMOJA WAINJILISTI ZAIDI YA 773 KANDA YA KASKAZINI AWAPA UJUMBE MZITO

Na Geofrey Stephen  Arusha

Katika kutimiza Miaka 60 ya KKKT na Jubilee ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Kanisa Dayosisi ya kaskazini kati umoja wa wainjilisti wakutana na Askofu wao  Doctar Solomon Masangwa .

Askofu wa KKKT dayosisi ya kaskazini Kati Ask.Dkt Solomon Masangwa amewataka watumishi wa Mungu kusaidiana ili kuongeza thamani katika huduma walizo nazo wakianza na familia zao

Askofu Solomon Masangwa Akifungua Mkutano wa Umoja wa Wanjilisti kandaya Kaskazini 

Ameyasema hayo leo katika mkutano na Baba askofu na wainjilisti wote wa dayosisi ya kaskazini kati uliofanyika usharika wa Ilkiranyi jijini Arusha

Askofu Amesema kuwa kusaidiana kunaanzia nyumbani katika familia na hatimae katika ngazi zote za jamii kwani kila mtu anapaswa kumtia moyo mwenzake ili kuujenga ufalme wa Mungu.

Picha ya Wainjiliti walio udhuria katika kikao hicho cha umoja wao wakisiliza kwa makini 

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wainjilisti dayosisi ya Kaskazini Kati Mwinjilisti Baraka Mollel amesema Lengo la mkutano huo ni kuzungumza na Baba askofu juu ya mambo mbalimbali yanayohusu huduma ya uinjilisti na ili kuimarisha umoja wao.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wainjilisti Baraka Mollel akitoa neno kwa wainjiliti hao 

pia kuzungumzia baadhi ya mafanikio ya umoja wao pamoja na chamgamoto zinazo wakabili na Askofu kuzisikiliza na kuFanyia kazi kwa wote kwa pamoja katika umoja wao wanafanya kazi ya Mungu kuleta jamii kwa Mungu na kugusa matatizo yao kila wanapo fanya ibada zao za mara kwa mara

Askofu Solomon Masangwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa umoja wa wanjilisti kanda ya kaskazini 

Nae Mwinjilisti Joseph Peter akisoma risala iliyoandaliwa na umoja huo wa wainjilisti ametaja mafanikio waliyoyapata tangu kuundwa kwa umoja huo huku baadhi ya wainjilisti wakieleza Yale waliyojifunza kupitia umoja huo ambao umekua msaada kubwa kwao .

Mwinjilisti Peter akisoma risala ya umoja huo mbele ya Askofu Solom Masangaa pembeni ni wainjilisti wenzake.

Katika mkutano huo wamehudhuria wainjilisti zaidi ya Mia Saba kutoka katika majimbo yote ya Dayosisi ya Kaskazini Kati na kwa pamoja wameonyesha nguvu ya umoja huo kwa kukutana na kubadilishana mawazo namna ya kujenga umoja huo ambao umekua chachu kubwa tangu kuanzishwa kwake .

+q

Msaidizi wa Askofu akisema neno juu ya umoja huo wa wainjilisti ambapo amesisitiza hmoja huo kudumu na kua na nvguvu ya pamoja na kuwataka kudumisha umoja huo  

Mwisho .