Site icon A24TV News

BARAZA LA TAIFA LA UJENZI LAENDESHA MAFUNZO KUSIMAMIA MIKATABA YA UJENZI.

Na Doreen Aloyce, Dodoma .

Dodoma Baraza la Taifa la ujenzi limeendesha mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi na utatuzi wa migogoro kat toika miradi ya ujenzi kwa wadau 155 kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani.

Mtendaji Mkuu wa baraza la taifa la ujenzi Dk.Matiko Mturi Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa baraza hilo katika serikali ya awamu ya sita.

Dkt Mturi amesema wameandaa Rasimu ya Mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara (base unit rates) kwa kila mkoa wa Tanzania bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya serikali ili kupata maoni na ushauri wao.

“Tunaendelea kuratibu utatuzi wa migogoro ya miradi ya ujenzi kwa njia ya adjudication na arbitration ambapo jumla ya mashauri 6 yametolewa uamuzi na 31 yanaendelea katika hatua mbalimbali za utatuzi” Amesema Dk.Mturi

Aidha Dkt Mturi amesema baraza limefanikiwa kuratib ,kuandaa na kuwasilisha Wizara ya ujenzi na uchukuzi(sekta ya ujenzi) andiko dhana (concept note) lenye mapendekezo ya kuboreshwa kwa mfumo wa sheria zinazosimamia ujenzi wa nyumba na majengo nchini.

Aidha mipango ya utekelezaji kwa februari 01 2023 hadi Juni 30 2023 kukamilisha kuandaa mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara kwa kila mkoa wa Tanzania bara na kupata maoni na ushauri wa wadau nje ya serikali hususani wakandarasi na washauri elekezi.
“Tunatoa mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi na utatuzi wa migogoro katika miradi ya ujenzi kwa wadau wa sekta ya ujenzi hususani taasisi za umma zinazotekeleza miradi ya miundombinu”Amesisitiza Dkt Mturi

Dkt Mturi amesema mwelekeo wa taasisi katika kutekeleza majukumu ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa sera ya ujenzi nchini,kuandaa na kutekeleza mpango mkakati wa maendeleo wa sekta ya ujenzi,kutoa miongozo mbalimbali ya kitaalam ya maeneo mbalimbali ya ujenzi.
Aidha ameongeza kuwa kuanzisha wiki ya huduma ya sekta ya ujenzi kwa wakati mmoja na kongamano la wadau wa ujenzi kwa lengo la kuimarisha uhusiano,ushirikiano hivyo kuongeza ubunifu na tecknolojia miongoni mwa wadau katika sekta hii.

Dkt Mturi amesema kuwa Taasisi inaendelea kutoa mafunzo kwa wadau wa ujenzi kuhusu maadili na utekelezaji wa miradi ya ujenzi, sanifu_jenga na usimamizi wa mikataba ya ujenzi kwa wadau mbalimbali pamoja na kutoa mafunzo yanayolenga kukuza na kujenga wataalam mahiri katika sekta ya ujenzi.