Site icon A24TV News

DKT MOLLEL ATOA MAJIBU MALALAMIKO UBOVU WA CHF.

Na dorin Aloyce Dodoma .

MFUKO wa Afya Ngazi ya Jamii (CHF) umelalamikiwa na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri (RMOs) kutokana na kutokidhi mahitaji ya wananchi kupata huduma za afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza leo Februari 20 2023, jijini Dodoma Mwenyekiti wa RMOs Dkt. Best Magoma wakati akiwasilisha risala yake kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel amesema CHF imekuwa ikilalamikiwa na wananchi namna ya utoaji wa huduma za matibabu wala upatikanaji wa dawa.

Akijibu risala hiyo, Dkt. Mollel amesema ni kweli kumekua na malalamiko makubwa ya wananchi kutokupata huduma zinazokidhi viwango kupitia kadi za CHF na kusema kwamba anakili CHF ni tatizo mila mahali anapofanya ziara na tayari Serikali inafanyika kazi suala hilo.