Na GeofreyStephen ,Arusha
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ,Missaile Musa amewataka wakurugenzi wa Halmshauri za Mkoa wa Arusha kubaini makundi au vikundi yanayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa zao ili kupata mafunzo kutoka Tume ya Ushindani (FCC) kwa lengo la kuongeza tija ikiwemo mnyororo wa thamani ,kwalengo la bidhaa kuwa na viwango kwenye ushindani wa soko.
Katibu Tawala wa Mkoawa Arusha Messaile Musa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa uwamasishaji .
Agizo hilo limetolewa Jijini Arusha na Katibu Tawala,Musa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uhamasishaji wa masuala ya ushindani na Udhibiti wa Bidhaa Bandia kwa wazalishaji Kanda ya Kaskazini.
Alisema endapo vikundi vinavyopewa mikopo na halmashauri vikipata mafunzo ya udhibiti wa ushindani wa kibiashara vitawezesha bidhaa zao kuingia katika masoko kutokana na ubora.
Lengo la kutoa maagizo ayo ni kukuza biasharana mnyororo wa thamani ikiwemo udhibiti wa bidhaa bandia na ukaguzi kwa walaji na wauzaji wa bidhaa mbalimbali.
Washiriki wakifatilia mkutano huo kwa makini wakati wa ufunguzi
“Wakurugenzi wa Halmshauri shirikianeni na FCC katika kuleta ushindani wa thamani za ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali wanaopata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na hlamshauri”
Naye Mkuu wa FCC Kanda ya Kaskazini,Nonge Juma alisema mafunzo hayo kwa wafanyabiashara wa viwanda vidogo vya kati na vikubwa yanalengo la kuwezesha kuleta tija katika ushindani wa biashara wanazozalisha ikiwemo kudhibiti bidhaa bandia zisizizosajiliwa na kuleta athari kiuchumi.
Mkuu wa kanda ya kaskazini Nonge Juma akizungumza katika mkutano huo
Alisisitiza wafanyabiashara hao na wenye viwanda kuhakikisha wanazongatia maadili ya biashara ili kuhakikisha soko linabaki shindani .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI),Anup Modha alitoa rai kwa wamiliki wa viwanda,wafanyabiashara mbalimbali kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuleta ushindani katika masoko kwa kuzingatia ushindani wa masoko wa ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa viwanda wa shirikisho la viwanda nchii bwanaAnup Modha akiwasilisha mada kwa washiriki