Site icon A24TV News

MIMI SIO MGENI SEPEKO MIMI SIO MGENI LEPURKO HAPA NI NYUMBANI “

Na Mwandishi A24Tv Arusha .

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilayani Monduli Ndugu Moitiko kisioki ameendeleea na ziara yake ya kata Kwa kata Kwa lengo la kushukuru, kukagua uhai wa wanachama ,kusikiliza kero za jumuiya hiyo pamoja na kutoa Elimu kwa viongozi .

Akizungumza katika ziara yake katika Kijiji cha Mti mmoja kata ya Sepeko hapo jana Amewapongeza Wananchi pamoja na wanachama wa kata hiyo kwa kuwa na mpango Bora wa ufugaji na kuwahidi kurudi kata hiyo kwa ajili ya Semina ya namna ya kuvuna majani(malisho) kupitia maeneo tengefu maarufu ilaliliak ili waweze kuvuna mifugo Yao kwa tija.

“Sepeko ni nyumbani tayari hapa Nina familia kwa maana ya Vikundi Kwa wamama , wamama Kuna mambo tuliyaongea Ile mbolea IPO kwa maana ya fedha na mnajua tutafanyia KAZI na ule mradi WA Sola Wale mama wawili waliochaguliwa kwenda Semina huko Kilimanjaro kwa ajili ya kujifunza nendeni mkajifunze mje muwafundishe wengine, na Kuna kikundi kilisemekana hakitambuliwi nawaaahidi tutafanyia ili kitambulike ” Mwenyeketi wazazi Monduli Ndugu kisioki.

Ziara hiyo amefanya pia katika kata ya Lepurko ambapo amesisitiza malezi kwa watoto.

” Wamama wa lepurko tukutane site mbolea ipo tukafanye kazi ,Mimi sio mgeni hapa , Sepeko wamenipokea vizuri hata hapa lepurko mmenipokea vizuri nawaahidi tuko pamoja na tutaendelea kuwa pamoja tukutane site”. Kisioki

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo Bi Bitrice amesema ili uwe mwanachama hai lazima uwe na kadi na lazima ulipe Ada ya mwanachama, huku akisisitiza malezi Bora kwa watoto.

 

 

Ziara hiyo ilianza rasmi wiki iliyopita katika kata ya LOORKISALE, LEMOOTI, NAALARAMI, SEPEKO NA LEPURKO huku akiendelea na ziara ya kata 15 zilizobakia katika Wilaya hiyo.