Site icon A24TV News

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMETOA MILION 33 KUNUNUA UNGA WA LISHE KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

Na Geofrey Stephen Arusha.

Halmashuri ya Jiji la Arusha limetoa kiasi cha Shilingi Milioni 33 kwaajili ya kununua unga lishe maalum kwaajili ya watoto wenye mahitaji maalum waliyopo mashuleni katika halmashauri hiyo lengo likiwa ni kuwaongezea afya ya mwili na akili kwa watoto hao.

Akikabidhi unga huo pamoja na vifaa vingine kwenye shule za msingi 9 ambazo zina idadi ya watoto 519 wenye mahitaji maalum Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Hargeney Reginald Chitukuro, amesema serikali kupitia halmashauri yake imefikia hatua hiyo ya kutoa vyakula vyenye lishe kwa watoto hao wenye mqhitaji maalum ili wazidi kukuwa kiafya na waweze kukuza taaluma zao wawapo darasani

“Naishukuru serikali kwa kuendelea kuwaangalia watoto hawa wenye mahitaji maalumu ili kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu. Hawawa watoto wanahitaji kukua kiakili na kimwili, pia wanahitaji viafaa mbali mbali vya kuwasaidia watoto hawa”. amesema Chitukulo.

“Sisi kama Jiji la Arusha tumesema tutaendelea kuwasaidia watoto hawa katika nyanja mablimbali ikiwemo ya miundombinu mashuleni ili iwe rafiki kwa watoto wetu hawa wenye mahitaji maalu”. ameongeza Chitukuro

Aidha Chitukulo ameeleza kuwa swala kuwanyanyapaa watoto wenye mahitaji maalum halitakuwa sawa maana nao pia wanavipawa kama watu wengine na wanaweza kuwa bora zaidi katika taifa hili na kulisogeza mbele katika hatua mbali mbali.

Niwaombe wazazi kuendeleza upendo kwa watoto hawa wenye mahitaji maalum tusiwafiche tuwatoe waje wachanganyikane na wengine kwenye kupata elimu bora nao wanayo nafasi ya kuifanyia jambo nchi yao maana wanavipawa vyao”. alisema Chitukuro.

Kwa upande wake Afisa mwandamizi kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia idara ya elimu maalumu Ndg, Seleman Chamshama amesema wao kama wizara wanaendelea kuhakikisha watoto wote wenye mahitaji maalum hapa nchini wanajiunga na masomo na tayari serikali ina3ndelea kuwaboreshea miundombinu ya elimu wawapo mashuleni.

“Yapo mahitaji mengi kwa watoto hawa ikiwamo sale za shule, viatu, madaftari n.k niwaombe watanzania wenzangu wenye kuguswa na hili waweze kuwasaidia watoto hawa ili waweze kupata mahitaji kama walivyo wengine kwasasa serikali tunahakikisha wanapata elimu ambayo itawasaidia na kukuza vipawa vyao”. amesema Chamshama.

 

“Niwaombe watanzania wengine wenye uwezo waweze kujitoa kuisaidia serikali kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum maana changamoto ni nyingi serikali peke yake haitaweza kumaliza ila kwa kushirikiana kwa pamoja tutaweza”. aliongeza Chamshama.

Aidha Chamshana aliipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Jiji la Arusha kwa kutoa fedha za kuwanunulia chakula chenye lishe watoto wenye mahitaji maalum kwa shule 9 ambazo zote zimepata unga huo pamoja ma vifaa vingine ambazo zinajumla ya wafunzi 519 ambao niwanufaika wa msaada huo. Pia amewapongeza wawazi wote waliyo watoa watoto wao ndani na kuwapeleka shuleni kupata elinu

Akishukuru kwa niaba ya walimu wakuu wa shule hizo 9 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kaloleni Mwalimu Miminini Payema amemshukuru Serikali kupitia Mkurugenzi wa jiji la Arusha kuguswa na kutoa chakula chenye virutubisho vyote vitakavyo saidia watoto kukua kiakili na kimwili

“Sisi kaloleni mpaka sasa tunao wanafunzi 128 wenye mahitaji maalum tunao wahudumia kuwapatia elimu hii ya msingi niwaombe wazazi wawalete watoto wenye mahitaji maalum ili waje wachanganyikane na wenzao kupata elimu sisi walimu tupo tayari kuwapokea na kuwapatia elimu bora”. Amesema Mwl Payema