Na Richard Mrusha
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam CPA Amos Makala leo februari 3,2023 amewakabidhi viongozi wa 12 tiketi za ndege kwenda nchni Rwanda kwa ziara ya mafunzo makabidhiano ya tiketi hizo yamefanyika katika ukumbi wa Dmdp ilala jijini Dar es salaam.
Pia Makala akachukua nafasi hiyo kuishukuru Benki ya NMB kwa kuwawezesha kupata tiketi za ndege 12 kwa viongozi wa 5 ambao ni wa wafanya biashara ndogo ndogo (Machinga) na 5 kwa viongozi wa bodaboda na mbili zikatolewa kwa wataalamu tiketi hizo ni za kwenda na kurudi.
Amesema viongozi hao wanatalajia kusafiri Feb 6,2023 kuelekea nchini Rwanda na kurejea nchni Tanzania Feb 10,2023.
Amesema Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo maalum ya kuweza kuyalea makundi ya machinga na bodaboda ambapo anachokifanya ni kutekeleza maono ya Mhe Rais.
Makala ameongeza kuwa kwa mkoa wa Dar es salaam kwa upande wa machinga na bodaboda wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na serikali ya mkoa katika mambo mengi ikiwemo Kuwapanga vizuri wamachinga kwenye shughuli zao ikiwemo usafi na kuweka utaratibu mzuri.
Ameongeza kuwa kwa upande wa bodaboda pia tumeweka utaratibu mzuri wa kutoa na kuingia mjini hiyo ziara ya mafunzo nchini Rwanda itawaongezea maarifa zaidi ambayo yatasaidia mkoa kupiga hatua zaidi katika mipango yake kama vile safisha pendezesha Dar es salaam,na kuwapanga vizuri wa machinga lakini pia kupanua fursa za kibiashara.
Ameongeza kuwa anatarajia kuona ziara hiyo inazaa matunda na kuwataka wamachinga na bodaboda kutumia fursa hiyo kutangaza biashara kwa vile Rwanda inategemea soko la kariakoo kununua bidhaa mbalimbali ambazo zinauzwa kwao.
Na kwa upande wake katibu wa machinga mkoa wa Dar es salaam Masudi Chauka (KIPANYA) amesema anashukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwawekea mazingira rafiki kwa shughuli zao.
Ndugu waandishi wa habari kama mnavyoona hiii leo kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa kushirikiana na Benki ya NMB tumekabidhiwa tiketi za ndege kwa ajili ya safari ya kwenda nchni Rwanda kwa ziara ya mafunzo ‘; amesema Chauka.
Ameongeza kuwa tunayofuraha kubwa kuona namna gani serikali kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa inavyoendelea kuwa nasi bega kwa bega hiii inaonyesha jinsi gani inavyothamini mchango wetu kama Kundi maalum na tutaendelea kuisapoti serikali kwa hali na mali.
Amesema tunaenda Rwanda kwa lengo la kujifunza lakini pia kuona fursa zilizopo uko na sisi tuweze kuzichangamkia kwa lengo la kutanua wigo wa biashara.