Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Baraka Kanunga amewataka wakazi wa eneo hilo kuachana na tamaa ya fedha na kutouza ardhi kiholela.
Kanunga ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa elimu ya afya ya uzazi wa mpango kwa kina baba na ahadi ya ukarabati wa madarasa ya shule ya msingi Komolo na ujenzi wa madarasa ya shule shikizi ya Olembole utakaofanywa na shirika la ECLAT Foundation.
Amesema ardhi ndiyo urithi wao uliobakia kwa jamii hivyo wakazi wa eneo hilo waachane na tabia ya kuiuza kwani aiongezeki ila binadamu wanazidi kuongezeka kila siku.
“Nawapongeza mno wanakwaya walioimba wimbo wakishika udongo na kuwausia wanajamii wasiuze ardhi nami naongezea hapo hapo kuwa ardhi ni mali msiuze,” amesema Kanunga.
MWISHO