Site icon A24TV News

TANESCO NCHINI KUTEKELEZA MIRADI YA UZALISHAJI UMEME, KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII

Na Doreen Aloyce, Dodoma

KATIKA kuimarisha miundo mbinu sekta ya umeme hapa nchini, na kuondoa changamoto kwa jamii, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema linatekeleza miradi ya uzalishaji iliyopo maeneo mbalimbali ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka, zitakazo patikana Megawati 5000 hadi 6000 ifikapo mwaka 2025 zitakazo uzwa ndani na nje ya nchi

Aidha Shirika hilo limesema haliuzi nguzo za umeme bali linauza huduma ya umeme kutokana na maneno ya wananchi ambayo yamekuwa yakisemwa bila uelewa wa kutosha .

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Martin Mwambene Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na utekelezaji wa shirika hilo.

“Najua Wateja wamekua wakijiuliza TANESCO hawafikirii kutafuta njia mbadala lakini sisi kama TANESCO tumefikiria kuwa na mbinu za miradi mbadala ambayo itaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme ikiwemo ya gesi na jua, pia kuna vyanzo binafsi vyenye uwezo wa kuzalisha umeme mfano viwanda vya sukari,”amesema.

 

Mwambene ameongeza kuwa TANESCO kwa kutambua matatizo ya umeme yaliyopo nchini imekuja na mradi wa Gridi Imara ambapo katika bajeti ya mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake.

Katika mradi wa Grid Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6000,mita laki 7za umeme, nguzo 380,000,ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa km 40,000, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takribani kilomita 948 na ujenzi wa vituo 14 vya kupooza umeme.

Aidha katika hatua nyingine Mwambe amezungumzia pia maendeleo ya ujenzi katika Bwawa la Mwalimu NYerere kuwa upo katika asislimia 88 na zoezi la uwekaji maji limefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.

“Kwasasa Mradi wa Umeme wa bwawa la Julius Nyerere upo asilimia 88 ambapo sasa hivi tumeanza kujaza maji ambayo yamefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.” Amesema Mwambe.

Mwsho .