Site icon A24TV News

TBA YATOA PONGEZI KWA SERIKALI KUTEKELEZA MAJUKUMU KWA UFANISI YAPEWA BILION 54.2

Na Doreen Aloyce,Dodoma

Mtendaji Mkuu wa TBA Daud Kondoro Amesema
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeishukuru serikali ya Rais Dkt. Samia kwa kukuendelea kuwawezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo kupewa fedha bilioni 54.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi.

Daud Kondoro ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa wakala huo katika kipindi cha miaka miwili.

“Naishukuru sana serikali ya Rais Dk. Samia kwa kuendelea kuiwezesha TBA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni Pamoja na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali. katika kipindi cha miezi 18, tayari imetoa sh. bilioni 54.2 ajili ya utekelezaji wa miradi,”amesema Kondoro.

 

Akizungumzia utekeleza wa majukumu ya TBA kwa mwaka 2021/22 2022/23 Kondoro ametaja miradi iliyotekelezwa kwa fedha za ruzuku amesema kuwa TBA ilipokea jumla ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 54.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi yake ikiwemoMradi wa Ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Dodoma.

Ametaja miradi mingine ni mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi jijini Dodoma,Ujenzi wa nyumba za Watumishi wa Umma katika eneo la Magomeni Kota, awamu ya kwanza na ya pili,Ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Temeke Kota ambapo linajengwa jengo la ghorofa 9 linalochukua familia 144.

“Umaliziaji wa ujenzi wa nyumba tano za majaji katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro, Mtwara, Kagera na Shinyanga, ambapo nyumba nne zimeshakamilika na kuanza kutumika,Ujenzi wa nyumba ya jaji Kagera unaendelea na umefika 30% ya utekelezaji huku Ukarabati wa nyumba 40 za viongozi jijini Dodoma, awamu ya kwanza na ya pili, Ukarabati wa nyumba 30 jijini Dar es Salaam,Ukarabati wa nyumba 66 za iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), pamoja na Ukarabati wa nyumba katika Mikoa 20 zilizohamishiwa TBA kutoka TAMISEMI.