Site icon A24TV News

WAKALA WA MAJENGO WAENDESHA ZOEZI LA KUWAONDOA WAIDAIWA SUGU WALIO KWEPA KULIPA KODI

Na Geofrey Stephen Arusha

Wakala wa Majengo Tanzania TBA imeanza kuwaondoa ndani ya nyumba wapangaji wake ambao ni wadaiwa sugu mkoa wa Arusha kutokana na Malimbikizo makubwa ya madeni yao kutoka kwa wapangaji walio kodi nyumba za shirika ilo .

Vyombo vya wadaiwa sugu zikitolewa nje na madalali walio pewa kazi iyo mara baada ya wadaiwa kukimbia na kuacha nyumba zao tupu .

Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo,kwa wapangaji watatu akiwemo mdaiwa sugu mwenye mwenye malimbikizo ayo kaimu meneja wa TBA mkoa sa Arusha ,Mhandisi Juma Dandi alisema kuwa operesheni hiyo ni ya nchi nzima na imelenga kukusanya fedha za serikali.

Naye dalali wa mahakama aliyepewa zabuni ya kukusanya madeni hayo ,kutoka kampuni ya udalali ya Twins Auction Mart Co LTD ya mkoani Rukwa ,Zuberi Lumbizi alisema kuwa mahakama.imewapa jukumu la kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu wa TBA na tayari mikoa sita nchini wameshaipitia.

Wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo wamilikinwa nyumba hawakukutwa kwenye nyumba na hivyo dalali alilazimika kuvunja milango na kutoa vitu nje kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa waliokuwa wakishuhudia zoezi hilo.