Site icon A24TV News

WANANCHI WATAKIW AKUACHA MIKOPO YA KAUSHA DAMU.

Na Doreen Aloyce, Dodoma

JAMII meshauriwa kuacha kukopa mikopo umiza kiholela Almaharufu Kama (KAUSHADAMU) na baadala yake wameshauriwa kuchukua fedha hizo kwa Matumizi lengwa kwani wanawake wengi wamekuwa wakichukua mikopo na kufanya mambo ambayo hayaingizi kipato kama vile kulipa ada,ujenzi wa nyumba na fahari za mavazi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Being’i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekekezaji wa majukumu ya baraza hilo .

Pia amesema kuwa watanzania wengi bado hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha itokanayo na mikopo na badala yake wanakopa bila kuwa na mipango waliyokusudia na kwamba pamoja na Serikali kutoa fedha za mikopo kiasi cha shilingi Trilioni 5.6 kwa ajili ya kuwawezesha watanzania milioni 8 bado watanzania wengi wanakabiliwa nakutokua na elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Nataka kuwaeleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana baraza kwa kushirikiana na serikali kwa ujumla wake wametoa kiasi cha sh.tirion 5 .6 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wapatao milioni 8 jambo ambalo ni hatua kubwa katika kuwawezesha watanzania kujiinua kiuchumi” ameeleza Beng’i.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa watanzania ili kuhakikisha watanzania wanajikwamua katika maisha na kuishi maisha ambayo yatakuwa bora kila mmoja jambo ambalo litawafanya watanzania kuwa na amani na furaha” amesema Beng’i.

Pamoja na hayo Beng’i amewashauri watanzania kutopenda kujitumbukiza kwenye masuala ya mikopo kama hawajajipanga kwa kujua wanachotakiwa kukifanya.

Aidha amewataka watanzania kuwa na nidhamu ya fedha sambamba na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba benki.

Vilevile amezungumzia ufanisi wa baraza hilo ambapo amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kihuchumi .

Katika kutilia mkazo juu ya kuwawezesha wananchi ameeleza kuwa kwa sasa kuna mifuko mbalimbali ya kuwawezesha akina mama na vijana huku akieleza kuwa akina mama wamekuwa wakipewa kipaumbele zaidi kwa kuwa ni waaminifu katika kurejesha.

Mbali na hayo amesema baraza limekuwa likisimamia kampuni za ndani kupata tenda Katika miradi mikubwa na yakimkakati inayoendelea hapa nchini ambapo jumla ya kampuni 1771 zimepatiwa tenda.
Mwisho.