Site icon A24TV News

WACHIMBAJI WADOGO 30 WASHIKILWA NA JESHI LA POLISI KWA VURUGU MIRERANI

Na John Mhala,Mirerani

Kikundi cha Wachimbaji Wadodo Wadogo zaidi ya 30 kutoka katika kampuni ya Gem$ Rock Venture Unaomiliki Mgodi Tanzanite Kitalu B  jana mchana wakiwa na silaha za jadi na majabali yenye ncha kali  wamevamia Mgodi wa Kitalu C na kujeruhi zaidi ya wafanyakazi kumi na wafanyakazi hao wako katika hali mbaya na wamekimbizwa hospital wakiwa mahututi.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara,Kamishina Msaidizi wa Polisi,George Katabazi na alisema kuwa baadhi ya watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi hilo.

Katabazi alisema ni kweli tukio hilo limetokea juzi mchana majira ya kati ya saa 6.30 hadi saa 8 mchana katika mgodi wa Kitalu B wa kampuni ya Gem $ Rock Venture na wahusika wako chini ya ulinzi kwa sasa na wanahojiwa polisi .

Kampuni ya Gem $ Rocky Venture inamilikiwa na Sammy Mollel ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara Wakubwa wa Kuuzaji na Kununuwa Madini Nchini {TAMIDA}.

Kamanda alisema kuna wachimbaji wa Mgodi huo wamekamatwa na wanahojiwa katika kituo cha polisi Mirerani na wengine wanasakwa ila hakuwa tayari kuwataka kwa kuwa anasema anaweza kuharibu upelelezi wa tukio hilo.

Kamanda alikiri kujeruhiwa kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Franone inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Onesmo Mbise maarufu kwa jina la Onee kwa kushirikiana na serikali lakini alidai kuwa hali zao si mbaya sana kwani wengine walipata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

‘’Tukio lipo na watu wamejeruhiwa na baadhi ya wahusika wamekamatwa na wanahojiwa polisi ila taarifa ikikamilika ntakupa taarifa’’alisema Kamanda Katabazi

Habari kutoka katika Mgodi wa madini ya Tanzanite Mirerani zilisema kuwa kundi hilo la wachimbaji haramu lililovamia chini kwa chini mgodi wa Kitalu C inadaiwa lilikuwa na lengo baya kwani lilikuwa na silaha za jadi na majabali{mawez] yenye lengo la kutaka kuwazuru wafanyakazi wa kitalu C ambao inadaiwa wamekuwa wakiwazuia kuingia kinyemela katika mgodi huo kuiba madini ya Tanzanite.

Vyanzo zaidi vilisema kuwa mpango huo umekuwa ukiratibiwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa Tanzanite ambao baadhi yao wana migodi Mirerani lengo ni kuhujumu jitihada za  mwekezaji mzawa na serikali kwa ujumla kutofanikiwa kuchimba kwa amani katika mgodi huo wa kitalu C.

Vyanzo vilisema kuwa hatua hiyo imefikiwa na wafanyabiashara hao kwa sababu Mwekezaji mzawa baada ya kufanikiwa kushinda zabuni iliyotangazwa na serikali na kuanza kazi alifanya kila namna kuziba mianya yote ya uchimbaji haramu maarufu kwa jina la BOMU inayoingia katika Mgodi wa Kitalu C hatua ambayo haikuwafurahisha wafanyabiashara hao kwani asilimia kubwa walikuwa wakichimba kinyemelea ndani ya Mgodi huo.

Mmoja wa wachimbaji ambaye aliomba kutotajwa jina lake alisema Rais Dkt Samia suluhu Hassan aliwahi kutamka kuwa Mgodi wa Kitalu C Unapaswa kulindwa kwa nguvu zote na anayediriki kuchimba kinyemela dola haitamwacha salama na kwa jinsi lilivyotokea juzi hao wavamizi wanapaswa kushitakiwa kwa kesi ya Uhujumu Uchumi.

‘’Shida ya Wachimbaji wa madini ya Tanzanite hawapendani na wana chuki na wivu sasa zabuni ilitangazwa lakini wengine walikaa kimya sasa hao hao wanampangia ajali mwezao hii ni hatari sana kuna siku itatokea mauaji’’

‘’Tunaomba sana serikali imlinde mwekezaji Mzawa afanye kazi kwa amani na wale wenye nia ovu serikali isisite kuwachukulia hatua kwa kuwa Rais alishasema’’alisema mchimbaji huo

Mwisho