Site icon A24TV News

BRIGEDIA THOMAS MUNISI,ACHUKUA FOMU YA MNEC KWA KISHINDO,KUSHUKA NA CHOPA KWENYE USAHILI

Na Geofrey Stephen Arusha .

Thomas Munisi akiwa katika Mavazi ya chama kikamanda zaidi 

Kada wa chama chamapindhzi Ccm Thomas Munis maarufu kwa jina la Brigedia munisi achukua na kurejesha form ya kugombea nafasi ya halmashauri kuu ya Ccm Taifa (Nec) Munisi kwa sasa ni Mwenyekitii wa Ccm kata ya themi na ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya Ccm wilaya ya Arusha ni mjumbe wa mkutano Mkuu Ccm Mkoa wa Arusha amekuwa Makamu mwenyekiti Taifa wa wafanyabiashara wa madini tanzania na ni mchimbaji na Mfanyabiashara maarufu wa madini na utali tanzania bara na Zanzibar.

Munisi licha ya kujaza fomu yake kwa utulivu wa hali ya juu Pia aliwahi kugombea nafasi mbali mbali ikiwemo nafasi ya  Ubunge ndani ya Ccm Jimbo la Arusha Mjini mwaka  2015 akashika nafasi ya Tatu kwa kishindo  kati ya wagombea wenzake 15
Na mwaka 2020 aligombea tena akashika nafasi ya 10 Kati ya wagombea wenzake 95.

Mpaka sasa Munisi ni Miongoni mwa wanasiasa nguli mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Arusha na ni miongoni mwa wafia chama wenye mvuto zaidi akiwa jukwaani  ukiljnganisha na wanasiasa wengine hivyo wenda akawa miongoni mwa moja wapo watakao peperusha nafasi ya mnec mara baada ya usaili kupita na usishangae msomaji wa A24tv akawa kinara  .

Mwisho