Site icon A24TV News

DIWANI WA BARAY ELITUMAIN, ACHUKUA FOMU YA UNEC NA KUREJESHA

Na Pamela Mollel Arusha .

Diwani wa Kata ya Baray Wilayani Karatu. Mhe Elitumain Magnus leo tarehe 25 March amechuku na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Mjumbe wa NEC Mkoa wa Arusha.

Elitumaini ni mtaalamu katika maswala ya uongozi na mahusiano ya jamii akiwa na shahada ya juu kutoka chuo kikuu cha Mzumbe.

Kiongozi huyo ambaye kwa Sasa ni Diwani wa kata ya Baray Wilayani Karatu, amewahi pia kushika nyadhifa mbali mbali katika chama cha Mapinduzi Ikiwa ni pamoja na Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji jumuiya ya vijana Wilaya ya Karatu na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa wa Arusha.

Kabla ya kutimkia katika Siasa amewahia pia kufanyakaza na mashirika ya kimataifa, nafasi zilizompa uzoefu katika maswala ya uongozi na utumishi kwa wananchi.

Hata hivyo akizungumza na chombo hiki, hakupenda kueleza malengo yake ya kugombea bali alieleza kuwa Chama cha mapinduzi kina makada wengi wazuri na wenye uwezo naye akiwa miongoni mwao hivyo vikao vya uteuzi vitakapopendekeza jina lake ndio utakua wakati sahihi wa kuzungumza dhamira na malengo yake kwa nafasi hiyo.