Site icon A24TV News

MENEJA WA MGODI WA GEM $ ROCK AENDELEA KUSOTA POLISI YEYE NA WENZAKE 21 KUPANDISHWA MAHAKAMNI MUDA WOWOTE KWA KUVAMIA MGODI WA KITALU C

Na John Mhala,Mirerani

Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture,Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti ametiwa mbaroni na wenzake 21 na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kwa tuhuma za kuongoza genge la Wachimbaji wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wana Apollo na kuvamia kinyemela ndani ya mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Kitalu C katika Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro.

Mgodi wa Kitalu C unaochimbwa kwa ubia kati ya Serikali na mwekezaji mzawa Onesmo Mbise ulivamiwa marchi 12 mwaka huu majira ya kati ya saa 6.30 na saa 8 mchana na kundi hilo wakiwa na silaha za jadi na majabali makubwa yenye ncha kali na kufanikiwa kuwajeruhi zaidi ya wafanyakazi 10 wa kampuni ya Franone ambao hali zao bado ni mahututi na wako katika hospital ya rufaa ya KCMC ya Mjini Moshi Mkoani Kilimanjro.

Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara,Kamishina Msaidizi,George Katabazi alisema kuwa polisi imefanikiwa kumkamata Saitoti ambaye inadaiwa kuwa ndio kiongozi Mkuu wa uvamizi huo na bado anahojiwa katika kituo Kikuu cha Polisi Mirerani.

Katabazi alisema mbali ya Saitoti kuna wana Apollo wengine wamekamatwa ambao ni wafanyakazi wa Kampuni ya Gem & Rock Venture,kampuni inayomiki mgodi wa Tanzanite ulipo kitalu B mpakani wa mgodi wa Kitalu C unaochimbwa na kampuni ya Franone unaomilikiwa na Mbise.

Kampuni ya Gem & Rock Venture unaomiliki Mgodi wa Tanzanite uliopo Kitalu B unamilikiwa na Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha,Sammy Mollel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wauzaji na Wanunuzi wakubwa wa Madini ya Tanzanite Tanzania{TAMIDA}.

Alisema kama taratibu za upelelezi na mahojiano zikikamilika huenda wakafikishwa Mahakamani mapema kujibu mashitaka lakini ikishindikana basi watafikishwa mahakani kesho.

‘’Tumemkamata Saitoti ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Gem & Rock Venture na pia ndio aliyekuwa kiongozi wa kuongoza genge la wavamizi katika mgodi wa serikali na mbia mwenza’’alisema Katabazi

Mkurugenzi wa Kampuni ya Franone unachimba mgodi wa kitalu C alisema kuwa yeye kwa sasa hawezi kusema juu ya tukio hilo na kusema kuwa ameiachia polisi kushughulika na wavamizi hao wenye ni ovu kwake.

Mwisho