Site icon A24TV News

MRITHI WA MREMA WA TLP KUPATIKANA KESHO UCHAGUZI WAPAMBA MOTO

 

Makao Makuu ya Tanzania Labour Party yalioko Magomeni usalama. 

Wanachama wa chama cha Tanzania Labour Party wanatarajia kumpata mwenyekiti mpya atakaye kiongoza chama hicho mpaka mwaka 2025 kabla ya mkutano mkuu kufanyika
Rasmi kumpata mwenyekiti Mpya

Uchaguzi huo utafanyika kesho tahe 06 mwezi wa 3 mwaka huu wa 2023 mara baada ya aliyekua mwenyekiti wa Tlp Mh Mrema kufariki Dunia mwaka jana mwezi wa nane 2022

uchaguzi huo unatarajia kutafanyika katika ukumbi wa mikutano ya Hotel ya Lego Hotel iliopo Sinza Jijini Dar es Salaam kuanzia majira saa tatu Asubui.

Wanachama kutoka Mikoa yote Tanzania bara na Visiwani zaidi 135 wenye sifa ya kuingia katika mkutano mkuu huo watapata fursa ya kupiga kura kumchagua mwenyekiti mpya wa Tanzania Labour Party Taifa .

Wagombea saba wamechukua Fomu za kugombea nafasi iyo ambapo mpaka kuelekea uchagui huo wagombea wapatao watano ndio walio rudisha fomu na zoezi limesha fungwa

Mwisho .