Na Mwandishi wetu, Kigoma.
Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amemuhakikishia mwekezaji wa kiwanda cha TROLLE MEES LE TANZANIA IVS LTD soko la uhakika la mafuta ya mawese baada ya kuanza utekelezaji wa kutatua changamoto zilizojitokeza kwenye ziara ya Mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe Kigahe ameyasema hayo Mkoani Kigoma wakati wa kupokea taarifa ya kamati ya kufanya tathimini ya changamaoto zilizojitokeza katika kuongeza thamani ya zao la mchikichi mkoani Kigoma.
Akiwa mkoani Kigoma mnamo tarehe 27 February ,2023 Mhe. Waziri Mkuu alipokea changamoto anuai kutoka kwa mwekezaji anajenga kiwanda cha kuchakata na kuongeza thamani mafuta ya mawese cha TROLLE MEES LE TANZANIA IVS LTD kinachomilikiwa na Bw. Abdalah Mwilima.
Aidha changamoto zilizoainishwa na mwekezaji huyo ni pamoja na upungufu mali ghafi ya zao la mchikichi, serikali impatie eneo la kupanda zao la mchikichi ili kuwa na malighafi ya kutosha ,
Vilevile umeme uliopo eneo la kiwanda kutokuwa na nguvu kidogo (low power) ya kutosha kuendesha mitambo iliyofungwa kiwanda hapo, hivyo kuomba Tannesco Mkoa wa Kigoma kufu
nga Transformer kubwa eneo la mradi, kutopata kiasi chote mkopo alichoomba katika benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) hivyo kuomba serikali imsaidie kupata mkopo huo kwa wakati.
Kutokana na changamoto hizo ,Mhe Waziri Mkuu aliagiza Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kupitia taasisi zake ikiwemo SIDO kushughurikia changamoto zote zilizoanishwa na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.
Aidha kutokana na maelekezo hayo Wizara iliunda kamati ya kushughurikia changamoto hizo kupitia taasisi zinazohusika na mnyororo wa uchakataji wa zao la mchikichi kuanzia hatua ya awali ya uchakataji kumfikia mlaji . Taasisi zilizohusika katika kamati hiyo ni SIDO,WMA,TEMDO, CAMARTEC,TIRDO na TBS.
Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya kamati hiyo Mhe. Kigahe amemuhakikishia mwekezaji huyo kuwa Wizara imepokea changamoto zote zilizoanishwa na kuzifanyia kazi kwa haraka sana huku baadhi zikiwa zimepatiwa ufumbuzi tayari na zingine zikiwa bado kufanyiwa kazi.
Naomba nikuhakikishie kuwa changamoto zote tumeanza kuzifanyia kazi baada ya kupokea maelekezo ya Mhe.
Waziri Mkuu.
“Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB) imeshafanyia kazi changamoto yako mambo ya kifedha limekamilika ,kuhusu Tannessco tumeongea na Meneja wa Tannesco Mkoa wa Kigoma changamoto hiyo inafanyiwa kazi kwa uharaka zaidi alisema Kigahe”
Awali akimkaribisha Naibu Waziri Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hasil Abdallah amemhakikishia Naibu Waziri utekezaji wa changamoto zilizoanishwa kwa kusema kuwa,yeye akiwa kama mtendaji mkuu wa Wizara atahakikisha zao la mchikichi linawakwamua wananchi wa Mkoa wa Kigoma kwa kuwa ndilo zao la kimkakati katika mkoa huo.
“Tunataka viwanda vyetu vitumie mafuta ghafi kutoka katika viwanda vyetu kikewemo kiwanda hiki cha TROLLE MEES LE TANZANIA IVS LTD Tunataka wakulima wanaozalisha mchikichi kutoka mkoa wa Kigoma wawe na uhakika wa kuzalisha zaidi, sababu soko litakuwepo la uhakika lakini hata mzalishaji atakuwa na uhakika wa kuzalisha zaidi maana atakuwa na uhakika ya malighafi” alisema Dkt Hashill.
Mwisho