Site icon A24TV News

SHEHENA LA MBOLEA ILIYO JAZWA MCHANGA YAKAMATWA WAZIRI ATOA MAAGIZO MAZITO

Na Mwandishi wa A24Tv .

Waziri wa kilimo Nchini Husein Bashe ameagiza kukamatwa kwa Mshindo Mbete msola Meneja mauzo kampuni ya mbolea ya Minjingu na Meneja wa kanda wa nyanda za juu kusini wa mamlaka ya kudhibiti mbolea Tanzania TFRA baada ya kukamatwa kwa mifiko 776 ya mbolea iyojazwa mchanga tayari kwa kuwauzia wakulima Njombe.

Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Njombe wamefanikiwa kukamata shehena hiyo ya mifuko 776 uliyo jazwa mchanga mithili ya mbolea ya minjingu tayari kwa kuwauzia wakulima mkoa wa Njombe.

Mshindo Msolwa ambaye Meneja mauzo wa mbolea za Minjingu ni miongoni mwa viongozi walio agizwa kuhojiwa na Waziri wa Kilimo Nchini Husain Bashe