Site icon A24TV News

TAZAMA MWENYEKITI WA WAINJILISTI, BARAKA MOLLEL ALIVYO MKUTANISHA ASKOFU WA DAYOSISI YA KASKAZINI KATI. ARUSHA NA WAINJILISTI 773

Katika Kikao  cha Umoja wa Waijilisti Arusha Mwenyekiti Baraka amesema anatamani aone mafanikio makubwa yanafikiwa na wainjilisti wenzake kuona wanapata bima za afya wote kuondokana na garama kubwa wanazo lipia pindi wanapo pata matatizo ya kiafya .

Akizungumza na A24Tv Mwenyekiti Baraka Mollel  amesema pia wanaomba kuboroshewa posho na pia zilipwe kutokana na watumishi mazingira wanayo fanyia kazi pamoja na kupata kwa wakati .

Katika umoja huo wainjilisti wameeleza changamoto kadhaa wanazo pitia nakuomba kufanyiwa utatuzi kwa lengo la kuendelea kufanya kazi zao kwa umakini zaidi ,

Wameeleza changamoto zao ni pamoja na wainjilisti wenzao kukataa umoja huo baadhi ya wainjilisti kipato chao ni kidogo ,wengine kushindwa kufanya  huduma kutokana  na kushindwa kuudhuria masomo ya thiologia

Matarjio ya umoja huo ni kuakikisha wanatatua changamoto walizo nazo na kufikia malengo makubwa ya umoja huo kusaidia kwa sehemu kubwa ya wainjilisti .

Mwisho .