Site icon A24TV News

TRA CHUNYA KUSAMBAZA ELIMU YA MLIPA KODI KWA WACHIMBAJI WA DHAHABU.

Na Richard Mrusha Chunya mbeya.

MAMLAKA ya mapato Tanzania TRA Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imesema kuwa asilimia kubwa ya mapato katika Wilaya hiyo yanatokana na Madini ambapo wachimbaji wadogo wamekuwa na uelewa mpana juu ya kifaa kinachotumika katika kurahisisha ukusanyanji wa taarifa za raslimali hizo.

Hayo yamesemwa na kaimu Meneja wa Mamlaka hiyo Osmund Mbilinyi wakati akizungumza kwenye maonesho ya kwanza ya teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Sinjiriri katika Mkoa wa Kimadini Chunya.

Aidha kaimu meneja huyo amesema kuwa lengo kubwa la kuwapo kwenye eneo la maonesho ni kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji pamoja na wateja wake wengine jambo ambalo itakuwa limerahisisha kusambaa haraka zaidi kwa elimu hiyo juu ya m lipa kodi.

“Wachimbaji wadogo ni wadau wetu muhimu pamoja na wanunuzi wa Madini hayo na kwamba sekta hiyo ndiyo inayotuingizia pato kubwa serikalini pamoja na mambo mengine hasahasa tunajikita kutoa elimu ya huduma za mlipa kodi kiganjani na watakuwa wanatumia huduma hiyo wao wenyewe pasipo kufuatwa na maafisa wa TRA,”amesema Mbilinyi.

Mbilinyi pia amesema kuwa TRA wapo katika kuboresha mfumo mpya wa mlipa kodi kiganjani ambao utamfanya mteja atafanya mwenyewe kila kitu, TRA itapitia kile alichokifanya mteja mwenyewe nakuongeza kuwa mbali na maonesho hayo pia TRA inao utaratibu wa kutoa elimu kila baada ya miezi mitatu kwa kuwafuata wafanyabiashara wa Madini pamoja na wachimbaji wenyewe kwenye maeneo yao ya kazi.

Amesema kuwa Mkoa wa Kimadini Chunya una masoko ya Dhahabu zaidi 20 ya ununuzi wa Madini hayo na kwamba TRA inahakikisha inafikisha huduma karibu na wateja wake na kufafanua kuwa elimu inayotolewa ni kuanzia ukadiliaji,usajili,uujazaji wa litany pamoja na shughuli zote ambazo zinaihusu TRA kwa wateja wake hasa wa Madini ambao ni Muhimu sana.

Mwisho.