Na Mwandishi wa A24Tv .Arusha
Ni katika Muendelezo wa Ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Monduli Ndugu Kisioki Lengoje Moitiko Katika kata ya Moita ambayo Jumla ya vikundi vilivyopo katika kata hiyo ni 47.
Akizungumza na Wanachama wa CCM na jumuiya zake ,ndugu Kisioki amesema lengo la ziara ni kushukuru baada ya kuchaguliwa na ni muendelezo wa ziara yake ambapo lengo kubwa ni kuwafikia wanachama wote , lakini pia kuwazesha Vikundi vya wanawake (vikundi,Vkoba) kiuchumi.
“Niwashukuru sana wanamoita kwani kati ya kata nilizotembelea yenye wanachama hai Moita ni Miongoni, lakini pia kina ma
Bitrice John Mandia ni katibu wa jumuiya hiyo Wilayani Humo , amesema ili uwe mwanachama hai lazima uwe na KADI ya Chama na Jumuiya zake , na kukusisitiza Umuhimu wa Elimu kwa Watoto wa Kike , na kuwasihi kina mama Kutoa taarifa sehemu husika pindi watakapogundua Mtoto wa kike kuozeshwa .
Prosper Damuni Meyani ni Diwani wa kata ya Moita ,yeye amesema Katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM, Serikali ya kata imesimamia kwa asilimia zote ikiwemo , ujenzi wa nyumba za Walimu Moita Bwawani,Umeme nk.
Nao baadhi ya wanachama na wananchi wa kata hiyo akiwemo Mwenyekiti wa UWT kata ya Moita wamemshukuru Kiongozi huyo wa Jumuiya ya wazazi kwa kutoa mwanga kuelekea mafunzo ya Ujasiriamali inayotarajiwa kuanza siku ya jumatano kuwa itakuaa chachu ya Maendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi kupitia miradi mbalimbali.