Waziri wa uchukuzi na ujenzi Profesa Makame Mbarawa ameridhishwa na ujenzi wa wakala wa majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Arusha.
Akizungumza mara baada kutembelea jengo Hilo katika ziara yake Mkoani Arusha amesema jengo Hilo libaendana na thamani ya fedha zilizotolewa ikiwemo Bilioni5.2 ambapo mpaka kukamilika litagharimu Kiasi Cha fedha za Kitanzania Bilioni 5 .
Kwa upande wake kaimu meneja TBA Mhandisi Juma Dandi amesema kuwa jengo hilo ambaloo ni kitega uchumi kutoka katika mamlaka hiyo ambapo mpangaji katika nyuma hiyo atapaswa kulipa Kwa wakati.
Alisema kuwa jengo Hilo litatumia mfumo wa Kitasa Janja Ili kuwabaini wadaiwa sugu Kwa hii itasaidia kuondoa usumbufu Kwa baadhi ya wapangaji ambao wanakuwa na malimbukizo ya madeni ambapo mfumo huo kamwe hautaruhusu mtu ambaye hajalipa kuendelea kuishi ndani ya jengo Hilo.
Hata hivyo jengo hilo linataraji kukamilika ndani ya wiki 2 au wiki3 ambapo jengo Hilo ni la ghorofa 10 na linatarajia kubeba familia 22.
Mwisho.