Site icon A24TV News

KIWANDA CHA KUTENGENEZA NGUO CHA JIJINI ARUSHA A,TO.Z YALAMBA TUZO KIWANDA BORA USALAMA MAHALA PA KAZI

Na Geofrey Stephen Arusha

Arusha.Kiwanda cha  kutengeneza nguo cha jijini Arusha A to Z  Textile Mills Limited , kimeibuka  na ushindi mzito wa kuwa kiwanda bora cha Usalama na Utunzaji wa Mazingira  mahala pa kazi na kushika nafasi ya pili kitaifa .

Akitoa tuzo hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Wenye Ulemavu Mh Prof . Joyce Ndalichako katika zoezi la siku ya Afya na usalama Duniani Kitaifa imefanyika Mjini Morogoro Mgeni Rasmi alikuwa Prof. Ndalichako.

Mh Waziri  amekipongeza kiwanda cha Ato Z kwa kutengeneza Mazingira mazuri ya Usalama mahali pa kazi na  kujali Mazingira na kutaka viwanda vingine kuheshimu usalama mahala pa kazi na kujali swala zima la Mazingira.

AtoZ ni Miongoni mwa viwanda vikubwa nchini ambavyo ni vinachangia pato pamoja na kulipa kodi kubwa serikalini na ni miongoni mwa viwanda vilivyo ajiri wafanyakazi wengi katika sekta ya viwanda binafsi .

Akipokea Tuzo hiyo  Meneja wa Maswala ya Usalama Afya na Mazingira mahala  pa kazi,Injinia  Harryson Rwehumbiza ambaye amewakilisha Kampuni kwa kuelezea mfumo nzima jinsi ya Kuwalinda wafanyakazi kuepukana na ajali  pamoja na magonjwa katika Kiwanda cha A toZ .

Meneja Rwehumbiza amesema kwamba kiwanda hicho kimeonyesha mbinu na mipango endelevu ya kazi katika kudhibiti wafanyakazi wasipate ajali za mara kwa mara kwa  kuanzisha semina mbalimbali huku  wakisimamiwa na Injinia Harryson Rwehumbiza ndiyo maana A to.Z imeibuka kidedea mshindi wa pili katika sekita ya viwanda vya nguo nchini.

Kiwanda cha ATo Z imekuwa  miongoni mwa vinara  viwanda ambavyo imeonekana havijakidhi vigezo hivyo Mh waziri amesisitiza kuendelea kujali swala zima la afya kwa wafanyakazi na kuondoa changamoto ambazo zinawakabili wanapokuwa maeneo ya kazi muda wote wawapo kazini huku wakihakikisha wanakuwa na vifaa muhimu vya kufanyia kazi na kutunza Mazingira.

Mwisho.