Na Wandishi wa A24tv .SIMANJIRO
Mashahidi 24 wa Jamhuri wanatarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya shambulio na kukaidi amri ya Wizara ya Madini inayomkabili Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha Joel Saitoti pamoja na Wafanyakazi wake sita wa mgodi wa Gem and Rock Venture uliopo Mererani.
Mwishoni mwa wiki katika mahakama ya wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali baada ya kubadilishiwa mashtaka katika tukio lililotokea marchi 13 mwaka huu katika mgodi uliopo kitalu B unaomilikiwa na kampuni ya Gem & Rock Venture.
Akisoma maelezo ya awali katika kesi ya shambulio inayowakabili washtakiwa sita Mwendesha Mashitaka wa serikali,Mosses Hamilton Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo ,Charles Uiso.
Alidai kuwa mnamo March 13 mwaka huu wafanyakazi sita wa Gem & Rock Venture waliwashambulia kwa Nondo, mawe ,Bereshi na Mabomba maofisa sita wa serikali waliokuwa ametumwa kufanya ukaguzi wa kawaida katika mgodi huo .
Maofisa walioshambuliwa ni pamoja na Besti Enosh,Vedastus Swea,Alvin Msuya,Swetbet Albogast na Maico Collman na kuwapatia madhara totauti mwilini.
Washtakiwa hao walikana kutenda kosa na upande wa Jamhuri ulidai kuwa utawasilisha mashahidi 16 na vielelezo vitatu na kesi imeathirishwa hadi Mei 10 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Washitakiwa hao sita ni Petro Exsaud(48) mkazi wa Moshono Arusha,Mosses Kelerwa(45) mkazi wa Mirerani,Daniel Siyaya (44) mkazi wa Ilboru Arusha, Mosses sirikwa (46) mkazi wa Ilboru,Dausen Mollel(58) Mkazi wa Ilboru na,Enock Nanyaro(32) mkazi wa Arusha kesi hiyo itakuwa na mashahidi 16 na vielelezo 6.
Wakati huo huo mwendesha Mashitaka wa Serikali Mosses Hamilton alidai kuwa shitaka lingine la kukaidi amri ya Wizara linamkabili Joel Saitoti na Enock Nanyaro litakuwa na mashahidi 8 na vielelezo 5 na mashahidi wanahifadhiwa hadi mei 10 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa katika mahakama hiyo.
Hamilton alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa Hilo wakati wakijua wazi kwa kufanya kosa hilo nikosa kisheria lakini washitakiwa wote walikana maelezo ya awali na dhamana yao iliendelea kwani kila mshitakiwa alidhaminiwa na mdhamnini mmoja na bondi ya sh,milioni moja.
Katika maelezo ya awali ya Mwendesha Mashitaka Hamilton mbele ya hakimu, Uiso alidai kuwa mnamo machi 13 mwaka huu, washitakiwa hao Saitoti na Nanyaro walikaidi kutii amri halali ya kusimamisha shughuli za uchimbaji iliyotolewa, Machi 13 mwaka huu na afisa mkaguzi wa migodi mhandisi Ezekiel Isaac .
Washitakiwa walikana shitaka hilo na dhamana ya mtu mmoja mmoja ilitolewa na kesi ilihairishwa hadi mei 10 mwaka huu itakapoanza kusikilizwa rasmi.
Ends…