Site icon A24TV News

MBUNGE JIMBO LA MWANAKWEREKWE ZANZIBAR HAJI ATOA PONGEZI KWA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU JIMBONI KWAKE.

Na Doreen Aloyce,Dodoma

Mbunge wa jimbo la Mwanakwerekwe Visiwani Zanzibar Khasimu Hassan Haji ameishukuru serikali kupitia Rais Samia suluhu Hassan na Dkt Hussein Ally Mwinyi kwa jinsi walivyoleta miradi ya maendeleo ya miundo mbinu jimboni kwake jambo ambalo limesaidia kuinua uchumi wa Zanzibar.

Kauli hiyo ameitoa Bungeni Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari juu ya maendeleo yaliyopo jimboni kwake kutokana na uchapakazi wa Serikali tofauti na hapo awali .

Amesema kuwa kupitia fedha ya Uviko 19 iliyoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani imeweza kujenga shule ya msingi ya ghorofa moja , mradi mkubwa wa maji na soko kubwa la kisasa.

Aidha amesema uwepo wa miradi hiyo inaenda kusaidia wananchi kuondokana na adha kubwa ya maji iliyokuwa ikiwakabili sambamba na watoto wao kupata elimu bora tofauti na hapo awali ambapo hapakuwa na shule za kutosha.

” Nina kila sababu ya kuishukuru Serilali yetu Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt Hussein Ally Mwinyi. kwa kutuletea maendelo makubwa wananchi wa jimbo la Mwanakwerekwe wakati nikiingia madarakani nilikuta jimbo linakabiliwa na changamoto za Shule ya Sekondari na Msingi , ubovu wa barabara za ndani,ukosefu wa maji na salama, na ufinyu wa soko ambalo linajengwa la kisasa kwa sasa,”

Kuwa kwa sasa watoto wanasoma katika mazingira mazuri, wananchi wanapata maji na hata barabara zinaendelea kukarabatiwa jambo ambalo litasaidia kuwa na usafiri wa uhakika wakati wa masika.

“Na uwepo wa soko la kisasa jimboni kwangu la mwanakwerekwe litasaidia kuinua uchumi wa zanzibar na biashara kwa ujumla na changamoto zilizopo mi ndogondogo za watu binafsi. “Amesema

Ametoa wito kwa wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki barabara zinavyojengwa huku wakitoa mashirikiano kwa makandarasi miradi inakamilika kwa wakati huku wakiwa walinzi kulinda miradi hiyo ili isiharibiwe.