Site icon A24TV News

NGUVU YA NGURUMO YA UPAKO YAMWANGUSHA MCHAWI NA UNGO ”NAOMBA NIPOKEE,NABII MKUU” SITAKI KUTENDA DHAMBI TENA

Na Mwandishi wa A24Tv .Arusha

Ungo uliotumika na mchawi  kusafiri kutoka Mbeya mpaka Arusha kisongo kwa Nabii Mkuu GeorDavie 

Mchawi aliyejitambulisha kwa jina la Maige Makwaya Mwenye Umri wa miaka 40 Mkazi wa Mkaoni Mbeya ameanguka na usafiri maarufu wa Ungo katika Viwanja vya kanisa la Nabii Mkuu Mh Dokta GeorDavie mara baada ya kuishiwa nguvu.

Akizungumza mara  baada kuishiwa nguvu na kuanguka chini mchawi huyo ameeleza kwamba ametumika kufanya kazi hiyo akiwa na umri  mdogo wa  miaka 10 mpaka sasa ana miaka 40.

Mchawi Maige akielezea zoezi lake la yeye kutoka mkoani Mbeya na kuanguka chini ya Kanisa la Nabii Mkuu Dokta GeorDavie

Kazi hii ya uchawi nimeanza nikiwa mdogo sana baada ya kuridhishwa na mababu zangu kutoka katika familia na hadi kufika kujisalimisha leo Arusha kwa Nabii Mkuu Mh GeorDavie kutaka kuokoka na kuachana na uchawi

Amesema amekua akifuatilia na kuona watu wakiponywa na kuamua kusafiri na ungo kutoka Mbeya hadi Arusha na ndipo alitaka kutua katika stend kubwa ya mabasi yaendayo mikoani na ndipo  aliogopa kushambiliwa na baadae kugeuza ungo wake na kuelekea kisongo ambapo alipo fika juu ya pawa la kanisa la Nabii Mkuu GeorDavie ambapo alishiwa nguvu na kuanguka chini .

Vifaa vya Mchawi mara baada ya kuanguka chini baada ya kuzidiwa nguvu 

Wakati anarudi kisongo alisikia nguvu ya ajabu imemwingia  na kumuangusha chini ndipo watu  wakaanza kumshangaa na kuanza kujiuliza alipo shukia ni wapi ? Na kujibiwa ni kanisani kwa Nabii Mkuu Dokta GeorDavie na baadae kupewa eneo la kukaa akisubiri utaratibu wa kupokelewa

Baadhi ya mashuuda wa tukio ilo wakizungumza na vyombo vya habari vilivyo fika hapo kujionea tukio ilo la aina yake wamesema kwamba majira ya saa kumi na moja asubui walisikia kishindo kikubwa nje na wasijue nini ndipo kutoka nje kumkuta mtu akiwa na usafiri wa ungo pamoja na vifaa vya kazi ikiwemo vibuyu na vitu vyeusi vilivyo fungwa vikicheza cheza .

Mkazi moja aliye jitambulisha kwa jina la David Joakimu mkazi wa kisongo  amesema yeye alimuona mchawi huyo akiwa amekaa katika msingi wa nyumba huku akishangaa na kuuliza ilipo madhabau ya Nabii Mkuu Dokta Geordavie ambapo alionyeshwa kwamba ni pale nyuma alipo kaaa umbali wa hatukua 5 mpaka saba na ndipo alienda huku nyuma akifuatwa na watu wengi sana wakisema amejisalimisha kwa Naabii achane na dhambi.

Mashuuda wa Tukio wakielezea namna mchawi alivyo anguka chini na Ungo lake mara baada ya kukutana na nguvu ya Nabii Mkuu Dokta GeorDavie 

Tukio hilo limegusa hisia za watu kwani wengi wao wamesema wamefuraishwa kuona kijana mwenye umri mdogo ameamua kuacha uchawi na kumrudia Mungu na kusema kwamba wanamuomba Baba Nabii Mkuu ampokee na kumwongoza sala ya toba na kuacha uchawi

Bibi kizee moja aliyejitambulisha kwa jjna la Martha alisema kuwa kila dhama na nyalati zake kuona kijana mdogo kusafiri na ungo kufuata ukombozi ni kutaka kufunguliwa na kuachana na ibada ya kimuungu amabayo imekua ikipoteza maisha ya watu kwa kutolewa kafara .

Wananchi wakimshangaa mchawi aliye anguka mara baada ya kuzidiwa na nguvu ya Upako wa Nabii Mkuu Dokta GeorDavie

Mpaka kituo hiki kinaondoka eneo la tukio Mchawi huyo alikuwa anasubiri ibada takatifu ya Nabii Mkuu kuanza majira ya saa saba mchana aweze kumuona na kumuelezea yalio msibu hadi kufikia kuanguka na ungo katika kanisa la Ngurumo ya Upako .

Mwisho.