Site icon A24TV News

SERIKALI IMEWATAKA WAONGOZA UTALII NCHINI KUTOA HUDUMA BORA ZA KITALII

Na Veronica Mheta,Arusha

Serikali imewataka waongoza watalii kutoa huduma bora za utalii ikiwemo uhifadhi wa mazingira ili historia iweze kuendelea kuwepo sanjari na kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania na maeneo mengine.

Aidha lazima vivutio vya utalii vilivyopo nchini lazima vitangazwe ili kukuza biashara ya utalii ili kuongeza idadi kubwa ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi.

Rai hiyo ilitolewa  Jijini Arusha na
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Dk, Hassan Abbasi kwaniaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa.

Alisema ni vema waongoza watalii hao wakatoa huduma bora ikiwemo kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania kwai haikuwa kazi rahisi kuitangaza nchi ya Tanzania kupitia vivutio vya utalii lakini Rais Samia Hassan Suluhu alitenga muda wake kwaaajili ya kutangaza vivutio vya utalii kupitia filamu ya Royal Tour .

Aliitaka kada hiyo kuongeza kasi zaidi kutangaza vivutio vilivyopo nchini na kuviuza ili wageni wa ndani na nje ya nchi waje nchini Tanzania.

“Ile filamu ya Royal Tour imemuonyesha Rais Samia akienda kuvua baharini na kupiia filamu ya Royal Tour amewaheshimisha waongoza utalii nchini hivyo msiwe wanyonge tafuteni vivutio vilivyopo mvutangaze kisha watalii waje nchini ”

Alisema serikali itachakata na kuwekeza fursa za utalii katika matukio muhimu yatakayotokea ndani na nje ya Tanzania na kusisitiza Tanapa kuendelea kutoa semina zaidi na taasisi ningine za utalii ili waongoza watalii waweze kujua mbinu mbalimbali zinazotumiwa ili utalii uweze kukua zaidi.

wakati Rais Samia alipotangaza nchi kupitia utalii walikaa zaidi ya saa tano kusubiri bahari itulie ili kuvua samaki na kutangaza vivutio vilivyopo katika uchumi wa buluu hivyo nanyi waongoza utalii msikate tamaa pambaneni kuhakikisha mnatengeneza fursa kupitia utalii

Alitoa rai kwa mamlaka za hifadhi kuangalia kwa karibu suala la wanyama kuongeza katika eneo la hifadhi wafungue njia za barabara ili kuwezesha wanyama kuonekana kwa karibu zaidi na kufikika

Alisema kupitia filamu ya Royal Tour watu bilioni 1.2 wameiona na kuijua nchi ya Tanzania ilivyo na vivutio vingi vya utalii na hii filamu imeanza kuleta watalii wengi nchini ikiwemo waongoza watalii kupata kazi nyingi zaidi.

“Tukio la Royal Tour liadumu miaka na miaka kwani imeojulisha dunia na kuwapata watu muhimu kujua nchi ya Tanzania ipoje na Rais alipokuwa nchini Marekani aliongea na waaandishi wa habari juu ya utalii uliopo nchini Tanzania na fursa nyingine mbalimbali na watu waliosoma magazeti hayo ziadi ya milioni 600 walisoma na kuifahamu vema nchi ya Tanzania”

Naye Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),William Mwakilema alisema Tanapa imejipanga kutangaza hifadhi tano ikiwemo Hifadhi ya Mkomazi ambayo awali zilikuwa hazitangazwi sana katika sekta hiyo ya Utalii.

Alizitaja hifadhi nyingine ambazo ni Saadani,Mikumi,Nyerere na Ruaha ambazo zimekuwa hazijulikani sana hivyo Tanapa imedhamiria kuzitangaza zaidi na kuziweka kwenye vifurushi vya safari za waongoza utalii nchini

Alisema utaratibu wa kufanya utalii katika vivuko vya nyumbu nakuazimia kwa pamoja waongoza utalii kuzingatia sheria na kanuni ikiwemo usafi wa mazingira kwa kwakushirikiana Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Tanapa na wadau mbalimbali wataandaa vipeperushi maalum vya kutunza mazingira.

Alisema kampeni yao ya” Discover Mkomazi ” itazinduliwa muda wowote kuanzia sasa yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii ambavyo havijatangazwa sana na kuagiza Tanapa kutoa mafunzo ya lugha zaidi za watalii kulingana na mataifa ya watalii wanaokuja nchini Tanzania ”

Naye Mwakilishi wa Waongoza Watalii Tanzania,Ridas Maiko Laizer amesema semina hiyo iliyoshirikisha waongoza utalii zaidi ya 1,302 ni chachu ya kuongeza idadi ya watalii milioni 5 ifikapo 2025 ambapo pia waliomba waongoza watalii hao kupata mikataba ya kazi ikiwemo viwango maalum vya malipo.

Pia maslahi ya waongoza watalii kiwango kisiwe chini ya dola za marekani 5O kwa siku kwani kampuni nyingi za utalii zinawatoza watalii fedha hizo lakini chaajabu waongoza utalii hawapewi fedha hizo lakini pia leseni za wangoza utalii wanaomba zifutwe kwani ajira hiyo si rasmi.

Aliomba vitambulisho vya vyama vya utalii vitumike badala ya vile vya makampuni na waliiomba serikali kuongeza kiwango cha fedha za bima ya Afya ili wanapoumwa waweze kutibiwa kuliko kuingia gharama kubwa za matibabu na kusisitiza wamiliki wa mahoteli watoe vipaumbele katika huduma za malazi ili nao waweze kulala mahali pazuri badala ya watalii pekee kulala ndani ya hoteli hizo.

Mwisho