Na Doreen Aloyce,Dodoma
Spika wa Bunge dkt Tulia Akson ameishukuru Bank ya Nmb kwakutambua umuhimu wa ibada ya kufunga kwakushiriki Iftari na wabunge pamoja na watumishi wa Bunge jambo ambalo linadumisha Upendo,Amani na mshikamano pande zote mbili.
Pia ameipongeza benk hiyo kwa kazi wanazofanya kama vile kurudisha faida kwa wateja kwakuchangia shughuli mbalimbali kama vile sekta ya elimu, afya na upandaji miti milioni moja nchi nzima.
Akizungumza katika viwanja vya Bunge wakati wa iftari iliyoandaliwa na bank ya nmb Dkt Tulia amesema kupitia iftari hiyo wamesikia mipango mbalimbali iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na bank hiyo kwaajili ya kuleta maendeleo katika jamii.
“Niwapongeze Nmb mmekuwa mfano bora hasa katika kudumisha umoja na tumeona mambo mengi mliyoyafanya niwasihi muendelee hivyo ili Taifa lisonge mbele” amesema Dkt. Tulia .
Aidha ametoa wito kwa bank ya nmb kutoa muongozo wa namna ambavyo wabunge wanaweza kupata miti na kupanda kwenye maeneo yao ili adhma ya kupanda mili milioni moja iweze kufanikiwa.
Awali akizungumza katika hafla hiyo Kaimu mtendaji mkuu ambae pia ni Afisa Mkuu wa biashara na wateja binasi Filbert Mponzi amesema kuandaa iftari hiyo ni katika jitihada za kuongeza ukaribu baina ya bank na wateja kwani mwaka huu 2023 bank ya nmb imetimiza miaka 25 tangu kuanza kutoa huduma
“Tunapofanya tukio hili ni kuongeza ukaribu na wateja wetu na tutaendelea kushikiana kadri tutakavyo weza ili iwe desturi yetu ya kila mwaka” amesema Mponzi.
Mwisho.