Site icon A24TV News

TCCIA MKOA WA ARUSHA WALIA NA HALMASHAURI YA JIJI ! KUPANDISHA KODI YA HUDUMA

Na Geofrey Stephen .Arusha

CHAMA Cha wafanyabiashara, wenye viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Arusha wamelalamikia Kodi ya huduma(service levy) inayotozwa na Halmashauri ambayo imepanda kutoka 0.03 hadi kufikia 0.3 jambo ambalo wamesema ni ongezeko kubwa.

Wakizungumza katika kikao Chao na mkurugenzi wa Jiji la Arusha mkoani hapa walisema ongezeko la Kodi katika biashara ni maumivu kwao na wakati mwingine inapelekea wafanyabiashara kufilisika na kushindwa kuendesha biashara zao.

Wafanya biashara wa jiji la Arusha wakifatilia mkutano kwa makini.

Mwenyekiti wa Chama hicho Walter Maeda alisema hawakatai Kodi hiyo ila wanaomba Halmashauri kuwapunguzia angalau ifike kwenye 0.1 lakini siyo 0.3 inakuwa mzigo mkubwa kwao na Kwa kuwa serikali ilitoa agizo Kwa Halmashauri kutoza isiyopungua asilimia 0.3 Wala isiyozidi kiwango hicho.

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Arusha Wolter Mahesa akizungumza na wafanga biashara wa Jiji la Arusha .

” Tunaomba Halmashauri Kwa kuwa ilipewa agizo la kutoza isiyozidi asilimia 0.3 basi itupunguzie angalau itoze kuendana na biashara husika inaweza kutoza hata asilimia 0.1 Ili isiwe mzigo kwetu wafanyabiashara”alisema Maeda.

Naye mdau mwingine ambaye ni mshauri wa Kodi kutoka Tax Point Consultant Simoni Lyakurwa alisema Kodi hiyo inaumiza Kwa kuwa ilitakiwa ichajiwe kwenye faida lakini ukipiga mahesabu ya asilimia tatu bado inakuwa Ipo juu ambapo alisema bado mamlaka nyingine zonachaji.

” Mapendekezo yetu ni hizi mamlaka ziangalie utozaji Kodi Kwa wafanyabiashara unakuta bidhaa moja inachajiwa Kodi nyingi kiasi Cha mfanyabiashara anazidiwa gharama za uendeshaji, Mfanyabiashara anachajiwa mpaka mara tatu kwenye faida yake jambo ambalo anaminywa zaidi”alisema Lyakurwa.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa jiji la  Arusha Joshua Myaluko alisema amefurahishwa kuona utayari wa wafanyabiashara hao wa kulipa Kodi ya huduma (service Levy) nakusema kuwa walichokiomba ni kuwekewa mifumo mizuri ya kuwahudumia ikiwemo kufikisha taarifa mapema ya kulipa Kodi.

Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha 

Mwishoooo.