Site icon A24TV News

VIJANA WAAGIZWA KUWA WABUNIFU KATIKA KUKUZA SOKO LA VIWANDA VYA NDANI

Na Geofrey Stephen .Arusha

Vijana wabunifu wameagizwa kutengeneza bidhaa zenye mahitaji sokoni ili kuwa na ubora zaidi utakaowawezesha kupata masoko na kuweza kujiajiri katika soko la ndani .

Agizo hilo limetolewa katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo(Sido) ,Jafari Donge wakati wa kufunga mafunzo ya wiki ya ujasiriamali na ubunifu yaliyofanyika chuoni hapo.

Alisema vijana wengi wanatengeneza bidhaa mbalimbali na serikali inatoa fedha kwaajili ya kuendeleza bunifu zao hivyo ni vema sasa wabunifu vijana wakatengeneza bunifu zenye mahitaji sokoni ili kujikwamua kiuchumi.

Alisema Sido na chuo hicho wanashirikiana katika kuhakikisha wabunifu wanatumia ziatamizi vilivyopo sido ikiwemo kuhuisha teknolojia na kuwatafutia masoko wajasirimali ili kupata masoko ndani na nje ya nchi.

“Vijana tengenezeni bidhaa zenye mahitaji sokoni ili mpate masoko ndani na nje ya nchi lakini pia bunifu zenu ziwe zenye tija.

Naye mshindi wa kwanza wa shindano hilo,Prisca Anthony alisema ameonyesha bunifu maalum ya video inayoonyesha tafiti mbalimbali za vijana wa ndani na nje ya nchi kabla ya kuomba kazi au kubuni bunifu mbalimbali wanapaswa kufanya nini ili kuendeleza vipaji walivyonavyo.

Awali Mratibu wa Kituo Cha Ujasiriamali wa Chuo cha ATC,Donatha Mwase alisema kuwa vijana 24 walishiriki kuonesha bunifu zao na wabunifu watano sh,milioni 2.5 kila mmoja kwaaajili ya kuendeleza bunifu zao kutoka hatua ya wazo hadi katika kitu kinachoonekana na kusisitiza kuwa washindi hao watapata sh, milioni 12.5 ya kwaaajili ya motisha wa kuendeleza bunifu zao.

Mwisho