Site icon A24TV News

VIJANA WAONYESHA IGIZO LA YESU LIVE KATIKA KANISA LA KKKT ,USHARIKA SALEI! YESU ACHAPWA KWELI KWELI

Ikiwa leo ni ijumaa kuu kwa wakristo kote nchini kanisa la Kkkt Usharika wa Salei Jijini Arusha umeadhimisha ibada iyo kwa vijana kufanya igizo la mateso ya Yesu live kuanzia Mwanzo mpaka mwisho

A24Tv ilikua ibadani hapo kufuatilia matukio yote na hapa ni picha za matukio ya igizo la bwana  Yesu

Bwana Yesu wakati wa igizo akiwa amepanda mwana Punda tayari kwa safari ya kuelekea Yerusalem 

Picha za igizo la bwana Yesu akiwa ameingia mji wa Yerusalem akiwa na wanafunzi wake na kuanza kuwafundisha masomo gafla wazee wa baraza waka mvamia katika mafundisho yake.

 

Wazee wa Baraza wakimuuliza yesu maswali mbali mbali kuhusu kufanya mafundisho kwa wanafunzi wake na jamaa wa Yerusalem na kwamba kibali amekipata wapi

Wazee wa Baraza wakimuuliza yesu maswali mbali mbali kuhusu kufanya mafundisho kwa wanafunzi wake na jamaa wa Yerusalem na kwamba kibali amekipata wapi.

Picha ya igizo bwana Yesu akiwa anapata karamu na wanafunzi wake kabla ya kifo chake.

Picha ya kahaba akimpaka yesu mafuta na wanafunzi wake wakimlalamikia juu ya kahaba mwenye dhabi kumkaribia , huku yuda akionyesha kumsaliti Yesu

Picha ya kahaba akimpaka yesu mafuta na wanafunzi wake wakimlalamikia juu ya kahaba mwenye dhabi kumkaribia , huku Yuda akionyesha kumsaliti Yesu.

Yuda Alivyo Msaliti na Kumuuza  Yesu kwa Baraza la Wazee kwa vipande 30 

Baraza la wazee likiongozwa na mkuu wa makuani Kayafa wakipanga namna ya kukamata Yesu na Kumsulubisha mara baada ya Yuda kumuuza kwa Viapnde 30 .

Yesu alivyo kamatwa na jeshi la askari na kuplekwa kwa Pilato ili asulubiwe mara baada ya Yuda kumsaliti na Petro kukana mara tatu 

Yesu mikononi mwa Pilato na kuamru apelekwa kwa Erode Mwenye Jimbo lake nchini Yerusalem kupata kibali cha kusulubiwa .

Mfalme Erode alivyo mziaki Yesu kwa kujiita Mfalme na kuamuru atandikwe bara bara na kurudishwa kwa pilato kutoa amri ya kusulubiwa 

Pilato alivyo nawa mikono yake na kusema damu  Yesu isiwe juu yake na kuagiza kutandikwa na kukabidhi kwa baraza la wazee na askari kwenda kusulubiwa ambapo askari na baraza walisema damu ya Yesu iwe juu yao wao na watoto wao na ndipo Yesu kuanza safari ya mateso msalabani 

Picha za Yesu alivyo beba msalaba na kuanza kusulubiwa na kuvuliwa nguo na kuanza kuwambwa  msalabani .

Yesu Juu ya Msalaba yeye na waalifu wawili huku wanafunzi wake wakimlilia juu ya mateso aliyo yapata .

Mwili wa Yesu ukiondolewa msalabani na kwenda kuwekwa kaburini mara baada ya mkuu wa makuani kuomba kwa Mfalme Pilato na kuagiza mwili huo kulindwa katika kaburi lake .

Mwisho