Site icon A24TV News

ASKOFU MASANGWA AWATA VIONGOZI WADINI KUSHIKAMANA KTK KUDUMISHA MAUSIANO

Askofu wa Kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini Kati Ask.Dkt Solomon Masangwa amewataka watumishi wa Mungu  kuendelea kua na mshikamano katika kutangaza kazi ya Mungu na kuonyesha umoja na sio kutengana katika kufikisha injili kwa waumini.

Askofu Masangwa ameyasema ayo wakati wa ibada maalum ya kuwaaga watumishi wa Mungu wapatao 34 kutoka Jimbo kuu la Morogoro ibada iliofanyika katika Usharika wa Salei , Levolosi ambapo watumishi hao walifika Mkoani Arusha kwa ziara ya kutangaza injili pamoja na kujenga mausino katika Dayosisi ya Kaskazini kati na sharika zake. kwa muda wa siku tano .

Masangwa amesema katika kipindi hiki anaomba kuona watumishi wa Mungu wanakua na Mshikamano na kutoa maubiri ya kujenga jamii ya wakristo na sio kutengana katika kazi ya Mungu .

Askofu wa Kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini Kati Ask.Dkt Solomon Masangwa akisema neno juu ya wageni kutoka Mkoa wa Morogoro .

Naye Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Salei , Levolosi Mchungaji Isaya Sessat amesema kwamba wamejisikia faraja kupata ugeni mkubwa wa  Wainjilisti kufika katika kuendeleza mausiano ambayo wamekua nao kwa muda mrefu ambao pia wamekua nayo kwa muda sasa mara baada ya kuanzishwa na wainjilisti 250 wa jimbo la Dayosisi ya kaskazini kati .

Amesema watumishi hao wamepata Fursa ya kutembelea vivutio mbali mbali ikiwemo ifadhi ya Manyara , kutembelea miradi inayo simamiwa na Dayosisi na sharika ikiwemo Shule Hospital na miradi mbali mbali pamoja na kufanya ibda ya nyumba kwa nyumba katika familia za waumini wa sharika walizo pangiwa .

Mchungaji kiongozi wa usharika wa Salei Mchungaji Isaya Sessat akitoa neno juu ya wageni waliofika ktk usharika wake .

Kwa uapande wake mkuu wa msafara huo wa watumishi wa Mungu akiongozana na wainjilisti Katibu Mkuu wa Jimbo la Morogoro Mchungaji  Paulo  Thomas amesema ziara yao imekua ni ziara ya kujifunza zaidi kutokana na Dayosisi ya kaskazini kua ni Dayosisi ambayo imepiga atua katika maendeleo na uwendeshwaji wa sharika kisasa .

Amesema wamepa fursa ya kutembelea miradi mikubwa inayo simamiwa na Dayosisi hiyo hivyo wamepata elimu kubwa namna ya wao kwenda kuenesha sharika zao pamoja na kusimamia miradi ya kanisa kwani wamejione mambo mengi mazuri ya kuiga katika kuendesha Dayosisi zao

Katibu Mkuu wa Jimbo la Morogoro Paulo Thomas  akitoa Salamu kwa Baba Askofu Solomon Masangwa .

Ibada hiyo iliudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo na waumini ambapo pia idara ya vijana ,wanawake na wajane walitoa zawadi kwa wageni wa Morogoro kama ishara ya upendo na kudumisha mausiano mazuri

Mwisho .