Site icon A24TV News

ELIMU YA VIPIMO NDIO MSINGI WA USALAMA WA CHAKULA NCHINI TBS

Na Ahmed Mahmoud
Imeelezwa kwamba Suala la elimu  Vipimo ni kiungo muhimu katika mnyororo mzima wa thamani na zana muhimu ya kuthibitisha ubora wa bidhaa hivyo elimu hii iende hadi vijijini Ili kusaidia makundi kuokoa jamii yetu.
Akifungua Maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani na hapa nchini Kwa Kanda ya kaskazini Jijini Arusha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Emmanuela Kaganda Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kwamba Ili usalama wa chakula Vipimo ni muhimu Sana Kwa watumiaji katika kuondoa changamoto ya utunzaji wa vyakula huko vijijini .
Ametoa Rai Kwa washiriki wa Maadhimisho hayo na Watanzania kuhakikisha vifaa vinavyotumika katika uzalishaji utoaji huduma na uchunguzi wa ubora vinafanyiwa uhakiki wa usahihi  Ili kufikia nchi kuwa na usalama wa chakula na  bidhaa zinazozalishwa au kuingia nchini.
Aidha Amesema TBS elimu hiyo ya vipimo isiwe Kwa wasindikaji lakini Kuna watu Moja Moja wanaojishughulisha na kilimo na kutunza vyakula ni muhimu elimu hiyo ikaenda hadi vijijini Tumesikia changamoto ya sumu kuvu basi elimu ni muhimu sana ikaenda hadi vijijini.
“Niwasihi TBS na Watanzania kupima mashine zenu katika kufikia uzalishaji wenye ubora utakaosaidia usalama wa chakula nchini mwetu na Kanda ya kaskazini kwa kutumia Vipimo sahihi Ili kukuza uchumi wetu na kuchukuwa hatua sahihi ya matumizi Bora ya vipimo”alisema Kaganda.
Awali akiongea kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa shirika la viwango nchini TBS Dkt. Yusuph Ngwenya alisema Vipimo ni kiungo muhimu katika suala Zima la ubora na usalama wa chakula ndio maana maabara zetu tumezigawanya katika makundi mawili ambayo ni viwanda na Sayansi.
Amesema siku ya Vipimo nchini ni sehemu ya Kutoa elimu Kwa umma juu ya suala muhimu la matumizi ya Vipimo hususani katika sekta za Afya viwandani na wafanyabiashara sanjari na wananchi kujenga mazoea ya kupima bidhaa zao.
Kwa Upande wake Joseph alisema maabara Yao imegawanyika katika makundi tisa ikiwemo uzalishaji wenye ubora kama mashine ni mbovu hivyo wao wanahakikisha ubora wa mashine kabla ya uzalishaji wa bidhaa
Amesema kwamba kama bidhaa wanazozalisha hadhikidhi viwango vya ubora hii itafanya bidhaa zinazozalishwa kuwa chini ya viwango na kushindwa kupata Ubora unaohitajika hivyo ni muhimu kuhakiki vifaa vya viwandani na mahospitalini.