Site icon A24TV News

KISHINDO CHA BENKI YA CRDB YATANGAZA ONGEZEKO LA FAIDA YA SHILINGI 351 BILIONI MWAKA 2022 TOFAUTI NA MIAKA YA NYUMA

Na Geofrey Stephen .Arusha.

BENKI ya CRDB  imetangaza ongezeko la faida ya shs,bilioni 351  mwaka 2022 baada ya kodi , ikilinganishwa na shs,bilioni 36 mwaka 2017 sawa na ongezeko la asilimia 875.

Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Arusha   wakati akizungumzia  maandalizi ya  Mkutano Mkuu wa 28 wa Wanahisa 2023 ambao utatanguliwa na semina ya wanahisa ambapo mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa, Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango Mei 20.

Mwenyekiti wa bodi ya CRDB, Dkt Ally Laay alisema kuwa katika miaka mitano iliyopita utendaji wa Benki umeimarika  licha ya kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa COVID-19 pamoja na vita ya Ukraine na Russia.

Alisema katika kukua kwa uwekezahi wa benki hiyo imafanikiwa kupata leseni ya kufungua kampuni tanzu ya CRDB  nchini DRC yenye thamani ya sh,bilioni 115 huku benki hiyo ikiwa na hisa ya asilimia 55.

Mpango mkakati wa miaka mitano wa Benki ya CRDB ni kuwa na matawi tanzu  katika nchi za Zambia,Comoro ,Malawi,Kenya na Uganda ambapo katika nchi ya Burundi  CRDB imefanikiwa kufungua tawi hilo mwaka 2012.

Awali mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ,Abdulmajid Nsekela alisema  nguvu kubwa ya benki hiyo ipo kwa wanahisa na kwamba hadi sasa benki ina wanahisa wapatao 39,000 wakiweno 10 kutoka kampuni na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa,benki hiyo imekuwa  na programu ya Imbeju ambayo imekuwa ikiwawezesha vijana na wanawake kuhusu maswala ya kuwezeshwa kiuchumi kwa kuwapatia mitaji kwa ajili ya kuendeleza biashara zao  pamoja na elimu kuhusu maswala ya fedha .

Aliongeza kuwa,wameweza kutoa elimu ya fedha sambamba na kutoa semina kwa vijana na wanawake Tanzania nzima kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Tume ya Tehama ,COSTECH ,Care International ambapo benki hiyo imefanikiwa kutoa kiasi cha 5 bilioni kwa ajili ya kusaidia wanawake na vijana.

“Tumetoa fedha hizo kwa makundi hayo ili kuwawezesha kufanya biashara zao na kuweza kurejesha kwa wakati  ili na wengine waweze kupata mikopo na kuendeleza biashara. “alisema .

Aidha alisema kuwa, katika kuelekea siku ya Mkutano Mkuu wa 28 wa Wanahisa 2023  itaenda na shughuli mbalimbali ikiwemo kugawa msaada wa madawati kwa shule ya Kilimani,kugawa pikipiki kwa kituo cha utalii cha polisi, pamoja na semina mbalimbali ambazo zitakuwa zinatolewa kwa vijana na wanawake pamoja na wanahisa kwa ujumla.

Mwisho .