Site icon A24TV News

LATRA YAKUTANA NA WADAU WA USAFIRISHAJI KUTOA MAONI JUU YA UBORESHAJI WA KANUNI MPYA ZA MAMLAKA

Na Geofrey Stephen Arusha
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Ardhini na Majini LATRA Imesisitiza kutokuwepo kanuni mahsusi zinazoonyesha utaratibu wa huduma za kintandao kama tiketi mtandao na mfumo wa ufuatiliaji wa mwendo vyonbo vya Usafirishaji kunaleta mkangwnyiko wa kushindwa Kutoa adhabu.
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Imesisitiza kuwa maoni ya wadau wa Usafirishaji ni muhimu Kwa lengo la utekelezaji wa majukumu ua shughuli za LATRA.
Akiongea  Mkurugenzi Msaidizi huduma za Usafirishaji wa Barabara Andrew Magombana wakati akifunga kikao cha wadau wa Usafirishaji kujadili mapendekezo ya kanuni mpya zilizoandaliwa chini ya Sheria ya LATRA sura 413 na sheria ya leseni za Usafirishaji sura 317 Kwa wadau wa  Mkoa wa Arusha .
Alisema kwamba Sehemu ya mabadiliko hayo ya kanuni ambayo yatatolewa maoni na wadau hao yatasaidia kuleta tija na kuondoa changamoto kadhaa zaidi ya 8 ikiwemo kutokuwepo Kwa kanuni ya usafirishaji wa bidhaa hatarishi Kwa Upande wa Barabara kama ilivyo kwenye usafiri wa majini na njia ya reli.
“Kuna kanuni ambazo hazipo mfano kanuni ya Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri Ardhini za Ufifishaji wa makosa za mwaka 2023  kanuni hizi zinalenga kufuata utaratibu uliowekwa na Ofisi ya mwendeshaji Mashtaka Mkuu wa Serikali kupitia sheria ya Mashtaka sura 430 katika kufifisha makosa”
Kwa Upande wake Meneja wa LATRA Mkoa wa Arusha Amani Mwakalebela Amesema kwamba siku ya Leo ni siku ya mchakato wa maandalizi ya kuandaa kanuni Kwa Kutoa  maoni  Kwa wadau wa Usafirishaji ndio lengo la kuwaita kwenye kikao hicho.
Alisema LATRA imeleta Kwa wadau hao mabadiliko ya Rasimu za kanuni Kwa ajili ya maoni yenu ikiwa ni sehemu muhimu katika mchakato wa kuandaa kanuni na kuwaomba wadau hao kutumia fursa na kuwa huru kujadili kanuni hizo Ili kuleta tija katika sekta ya Uchukuzi.
Kwa Upande wake Mwanasheria wa Latra Mwadawa Amesema kwamba Rasimu hiyo ya Ufifilishaji matumizi yake ni Kwa wadau hao hivyo ni fursa muhimu Kwao Kutoa maoni yatakayosaidia kuboresha na kuondoa changamoto za uendeshaji wa Latra nyingi zikiwa za uendeshaji wa iliyokuwa Sumatra.
Alisema kuwa Athari ya maslahi ya umma yatasimama kuliko Athari za mtu binafsi ikitambua suala hili ni la kitaifa Kwa makosa ya kufifilisha Kwani wanawajibu wa kupeleka mwendesha Mashtaka makosa ya kufifilisha kila baada ya miezi mitatu.
“Hakuna mabadiliko ya adhabu ila ni kwamba tumeweka kanuni za ufifilishaji Kwa Sababu ya kuboresha uthibiti wa Masuala ya makosa mbalimbali yanayotikea Kwa wasafirishaji nchini ikumbukwe Rasimu hizi ni mpya na zimetengenezwa chini ya kanuni ya 45 inayompa Waziri Mamlaka ya kuizinisha”
Mwisho.