Na Geofrey Stephen Arusha.
BENKI ya CRDB imeikabidhi Wilaya ya Arusha Madarasa ya kisasa mawili vyenye thamani ya sh,milioni 42 katika shule ya Sekondari Kilimaji ya Jijini Arusha hiliyopo katika kata ya Moshono yakabidhiwa katika Mkoa wa Arusha ikiwa ni jitihada za kuunga mkono serikali katika kuboresha miundo ya elimu Nchini.
Akiongea katika hafla hiyo ikiwa ni sehemu ya kuelekea mkutano mkuu wa 28 wa wanahisa wa CRDB, iliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo kata ya Moshono,jijini Arusha.
Katika muktadha huo benki ilipokea maombi ya uhitaji wa madarasa hayo katika shule hiyo ya sekondari Kalimaji iliyoanzishwa januari 2022 ikiwa na wanafunzi 58.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo alipokea ombi la Uhitaji wa jengo la maabara pamoja na vishkwambi kwa wanafunzi na kutoa mchango wa sh,milioni 10 kwa ajili ya maombi hayo.
Alitoa rai kwa uongozi wa shule hiyo kutunza majengo hayo ili yasaidie vizazi vijavyo ,pia aliwaomba wazazi kuwafungulia akaunti watoto wao ili kuiwezesha benki hiyo kujiendesha na kuendelea kuisaidia jamii.
Hata hivyo alisisitiza kuwa serikali ya awamu ya sita imewekeza zaidi katika sera ya elimu hasa ujenzi wa miundo mbinu ya madarasa na kuifanya elimu ya sekondari kuwa bure.
Awali mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo alitoa rai kwa wananchi kuweka uzalendo mbele kwa kuitumia benki CRDB kufungua akaunti ili kuinua uchumi wa taifa kwani benki hiyo imekuwa mahususi kurejesha sehemu ya faida kwa jamii.
Aliiomba benki hiyo kuona umuhimu wa kuendelea kuisaidia shule hiyo ambayo bado inachangamoto kubwa ikiwemo ujenzi wa jengo la utawala pamoja na uhitaji wa kompyuta kwa wanafunzi.